31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Idris awakwepa washiriki BBA Dar

IDRISNA THERESIA GASPER
MSHIRIKI wa Big Brother Afrika ‘BBA’ Hot Shot 2014 kutoka nchini Namibia, Luis Munana, amemwagia sifa aliyekuwa Miss Tanzania 2016, Wema Sepetu kuwa ni mwenye mvuto wa kipekee.
Lakini licha ya kutoa sifa hizo, mshiriki mwenzao ambaye ndiye mwenyeji wao, Idris Sultan, hakutokea katika sherehe hiyo jambo lililozua minong’ono kwa watu baada ya tetesi kwamba ana ugomvi na Wema Sepetu.
Wema alimwagiwa sifa hizo alipokuwa katika sherehe za Instagram Party katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Wasanii ninaowakubali kutoka Tanzania ni Wema Sepetu, ni mrembo sana nampenda, wasanii wengine ambao nawakubali ni Shilole, Ommy Dimpoz pamoja na wimbo wake wa Wanjera,” alisema.
Washiriki wengine wa BBA waliohudhuria sherehe hizo ni Nhalanhla na Samantha wote kutoka nchini Afrika Kusini.
Wasanii wa Tanzania waliohudhuria sherehe hiyo ni Ben Paul, Izzo Bizness, Shelta, King Majuto, Stan Bakora, JJ Band, huku mshereheshaji akiwa Adam Mchomvu, B Dozen na DJ Ommy.
Hata hivyo, Wema alishukuru kupendwa na Luis. “Jamanii sina hata la kusema jinsi ulivyonisifia, nashukuru sana sana,” alijinadi Wema akishukuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles