25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Shahidi kesi ya Zitto aeleza alivyotuma ujumbe kwa wabunge

Tunu Nassor – Dar es Salaam

SENGWE Mbarouk ambaye ni shahidi wa tatu katika kesi ya uchochezi inayomkabili Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alituma taarifa kwa wabunge wanne wa Mkoa wa Kigoma kuhusu mapigano kati ya wakulima na polisi yaliyotokea Kijiji cha Mpenta, Uvinza lakini yalifanyiwa kazi na wabunge wawili tu.

Akitoa ushahidi wake jana mbele ya Hakimu Hakimu  Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi,  alidai kuwa baada ya kupokea taarifa hizo aliamua kufanya hivyo kwa kuwa ndiyo wawakilishi wa wananchi.

Mbarouk alisema taarifa za mapigano hayo alizitoa kwa Mbunge wa Kigoma Kusini, Hasna Mwilima (CCM); wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba (CCM); wa Kasulu, Daniel Nsanzugwako (CCM) na Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo).

“Pamoja na kutoa taarifa hizo, Mbunge Hasna ndiye aliyezungumzia suala hilo bungeni na Zitto aliitisha mkutano wa waandishi wa habari,” alidai Mbarouk.

Alisema kuwa lengo lake la kutoa taarifa ni kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na Serikali ifanye uchunguzi kwa waliohusika wachukuliwe hatua.

Mbarouk ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wakulima alidai kuwa aliyemtaarifu tukio hilo alikuwa ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye alimfuata na kumwomba awasemee wakulima.

“Aliniambia kuwa ninyi ndio mnawasemea wakulima, basi kuna tukio la mapigano kati ya wakulima wenu na polisi linalosababisha watu wengi kuuawa,” alidai shahidi huyo.

Zitto anatuhumiwa kwa makosa matatu ikiwamo kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya polisi na wananchi anayodaiwa kuyatoa Oktoba 28, 2018.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles