30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Jafo akabidhi pikipiki kwa maofisa tarafa

Mwandishi Wetu – Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amekabidhi pikipiki 448 kurahisisha utendaji kazi kwa maofisa tarafa nchini.

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika juzi jijini hapa, Jafo alisema kuwa  kila mkuu wa mkoa katika eneo lake la kazi ana wajibu wa kuhakikisha pikipiki zinawafikia walengwa ambao ni maofisa tarafa kwa kuzingatia mgawanyo wa tarafa walizowasilisha.

“Simamieni na kuhakikisha kuwa pikipiki hizi na magari mliyopatiwa  hivi karibuni vinatumika kwa shughuli za Serikali katika maeneo yenu na si vinginevyo,” alisema Jafo.

Alisema kuwa matumizi ya chombo chochote ni muhimu na hivyo wakuu wa mikoa wahakikishe pikipiki hizo na magari waliyopatiwa hivi karibuni yanafanyiwa matengenezo kwa wakati.

Aidha Jafo  alisema kuwa vyombo hivyo vya usafiri vitadumu kwa muda mrefu na kuweza kutoa huduma kwa wananchi kwa urahisi ili kuongeza chachu ya maendeleo na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Ifahamike kuwa Serikali imetumia shilingi bilioni moja kwa ajili ya kununua pikipiki hizi, ni lazima zitunzwe vizuri ili zitumike kwa muda mrefu na kurahisisha utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi,” alisema Jafo.

Alisema kuwa Serikali ina vipaumbele vingi, hivyo ni busara  kuvitunza vyombo hivyo ili fedha inayopatikana iweze kuelekezwa katika vipaumbele vingine vya uwekezaji katika miundombinu na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika, alisema kuwa  pikipiki hizo zitarahisisha utendaji kazi kwa maofisa hao, hususan kipindi cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge, waliishukuru Serikali kwa kutatua kero ya usafiri kwa maofisa hao huku wakiahidi kutunza vyombo hivyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles