23.4 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

SETHI APINGA UONGOZI MPYA IPTL MAHAKAMANI

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM


SIKU chache baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), kumng’oa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Harbinder Sing Sethi, kiongozi huyo ametangaza kusudio la kwenda mahakamani kuupinga uongozi mpya wa kampuni hiyo.

Sethi ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, ametangaza uamuzi huo kupitia kwa mwanasheria wake, Hajra Mungula.

Sethi aliondolewa kwenye uongozi wa kampuni hiyo katika kikao cha bodi kilichofanyika Aprili 10 mwaka huu, Joseph Makandege aliteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mungula alisema suala hilo limekaa kisheria zaidi ndiyo maana wameamua kwenda mahakamani.

“Mimi nafanyia kazi maelekezo niliyopewa na mteja wangu hivyo, tunatarajia kwenda mahakamani kwa sababu hili suala liko kisheria zaidi.

“Inaweza kuwa kesho (leo), kesho kutwa au mtondogoo lakini ni ndani ya wiki hii,” alisema Mungula.

Alisema taratibu za kumwondoa Sethi hazikufuatwa kwani mteja wake hakufahamishwa chochote juu ya mabadiliko yaliyotokea.

“Tunaona taratibu hazijafuatwa na ‘forum’ sahihi ya kufanyia mabishano kwa kila upande ni mahakamani.

“Sisi wanasheria tuna sehemu maalumu ya kufanyia mabishano na kwa hapa tulipofikia tunaona mahakama ndiyo mahala salama kwa hiyo yale yaliyoibuliwa na mengine yatakayoibuka tutabishania mahakamani,” alisema Hajra.

Sethi ambaye bado yupo mahabusu alisema kupitia mwanasheria wake kuwa yeye bado ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.

Mungula alikaririwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akisema kuwa aliwasiliana na mteja wake ambaye yuko rumande na kushangazwa na taarifa za kung’olewa kwake.

Alisema licha ya kwamba Sethi bado yuko mahabusu akituhumiwa na mashtaka kadhaa ya jinai, hiyo haiondoi ukweli kuwa IPTL ni kampuni binafsi yenye wamiliki halali wenye hisa halali na wala si NGO ambayo mtu yeyote anaweza kutangaza mapinduzi ya kiuongozi wakati wowote.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles