26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

UKWELI ULINZI UKUTA MIRERANI

Na Masyaga Matinyi-SIMANJIRO


IKIWA zaidi ya mwezi mmoja tangu Rais Dk. John Magufuli,  azindue ukuta wa Mirerani, imebainika hakuna wanajeshi kutoka nchi jirani ya Rwanda wanaolinda ukuta huo.

Ukuta huo umejengwa kuzunguka machimbo ya madini ya tanzanite, yanayopatikana Tanzania pekee katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

Hivi karibuni kumekuwapo taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii, zikidai Serikali ya Tanzania imekodi wanajeshi kutoka Rwanda kwa ajili ya kulinda eneo hilo nyeti kwa uchumi wa nchi.

MTANZANIA ilipiga kambi katika machimbo hayo ya tanzanite yaliyopo Mirerani kwa wiki nzima, limethibitisha bila shaka kuwa maofisa na askari wa jeshi waliopo maeneo ya ndani na nje ya ukuta ni Watanzania kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Katika eneo la ukuta na maeneo mengine ya mji mdogo wa Mirerani, wanaonekana askari wa JWTZ na JKT wakiendelea na shughuli zao za kila siku, lakini hakuna askari hata mmoja aliyeonekana akiwa na sare tofauti na zile za askari wa Tanzania.

Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umegharimu takribani Sh bilioni 6 na ulijengwa na wahandisi na vijana kutoka JKT.

Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi, alisema Serikali haiwezi kujibishana na taarifa za kwenye mitandao ya kijamii.

“Mimi kama waziri siwezi kupoteza muda kujibu mambo ya kwenye mitandao, ndio maana suala hilo tumeamua kulipuuza na kukaa kimya,” alisema Dk. Mwinyi

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles