24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaziangukia taasisi za fedha, kilimo

1NA FLORIAN MASINDE, DAR ES SALAAM

SERIKALI imezitaka taasisi za kifedha na binafsi kuwekeza zaidi katika sekta ya kilimo ili kuchangia kuiinua na kuboresha uzalishaji.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la tatu la biashara na kilimo la Afrika Mashariki.

Alisema Tanzania kuna matawi ya benki zaidi ya 52 nchini nzima hivyo ni rahisi kwa wakulima kukopa fedha na kurejesha sambamba na kupata pembejeo bora za kilimo.

“Huu ni wakati mzuri kwa taasisi hizo kujikita zaidi katika kilimo kwa sababu asilimia 75 ya Watanzania wanategemea kilimo, ufugaji na uvuvi katika uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula,” alisema.

Kuhusu wakulima wadogo wadogo,  Turuka alisema kuwa Serikali kupitia sera ya uwekezaji, wakulima wamepewa kipaumbele kwakuwa wao ndio wawekezaji muhimu katika kilimo.

“Pia Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara, reli, maji na anga ili kuwarahisishia kusafirisha mazao yao na kupanua soko la ndani na nje kuweza kukidhi mahitaji na kuongeza kipato cha taifa,” alisema.

Hata hivyo, alisema bado kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya kilimo nchini zikiwamo ukosefu wa zana bora za kilimo, elimu ndogo kuhusu kilimo, mitaji na ukosefu wa masoko hivyo kusababisha sekta hiyo kudorora.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dk. Yusufu Sinare, alisema wataendelea kuandaa makongamano kama hayo mikoani ili kuwafikia zaidi wakulima na kuwaunganisha na taasisi nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles