23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 5, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAPANGA KUNUNUA VICHWA VYA TRENI VILIVYOZUA UTATA

Na CHRISTINA GAULUHANGA

SERIKALI  imeunda jopo la wataalamu 11 kuchunguza vichwa 13 vya treni ambavyo Rais John Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe Julai, mwaka huu, ili kama vitathibitika kuwa ni vizima serikali ivinunue.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa mashine za kukagua mizigo bandarini (scanner).

Alisema Serikali imekusudia kuvinunua vichwa hivyo vya treni kwa matumizi endapo vitakuwa ni vizima na kama havitakuwa na matatizo yoyote.

“Tukibaini kama vichwa hivi 13 kati ya 15 vina ubora tutakaa pamoja na wenye mali tuongee kama tutaweza kuvinunua,” alisema Mbarawa.

Uamuzi huo wa Serikali umekuja baada ya Rais Magufuli kuagiza uchunguzi ufanyike haraka juu ya aliyeviagiza vichwa hivyo.

“Kuna vichwa 15 vya treni vilishushwa hapa lakini havina mwenyewe. Inawezekana vipi vichwa vya treni vinafika hapa bandarini, vinashushwa lakini mwenyewe hajulikani! Ni kwa sababu hakuna coordination, huo ni mchezo mchafu. Vyombo vya dola vianze kuwachunguza hao,” alisema.

Licha ya vichwa hivyo kuwa na nembo ya Shirika la Reli nchini (TRL), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo alikana kumiliki au kuagiza vichwa hivyo.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, aliweka bayana kwamba, vichwa hivyo vina nembo ya TRL na kwamba ulitokea mgogoro kati ya shirika hilo na kampuni iliyotengeneza vichwa hivyo, baada ya kubainika kuwa mchakato wake wa ununuzi haukuwa sahihi.

Aidha, Septemba 12, mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola, alisema katika uchunguzi wao wamebaini mmiliki wa vichwa hivyo ni Kampuni ya Electro-Motive Diesel ya Michigan, nchini Marekani.

Mlowola, ambaye alikuwa akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Azam, alisema  baada ya uchunguzi wamebaini mchakato wa kununua vichwa hivyo ulishaanza tangu mwaka 2014/15.

“Lakini TRL na kampuni hiyo hawakufikia mwisho na hapakuwa na mkataba uliosainiwa wa vichwa hivyo kufika nchini au kununuliwa nchini na TRL. TRL ilishaanza mchakato wa ununuzi wa vichwa hivyo, lakini hapakuwa na mkataba wa vichwa hivyo.

“Kampuni hiyo walileta kwa matumaini huenda vitanunuliwa, licha ya kwamba hakuna mkataba wa mauziano kati ya hiyo kampuni na TRL, japo mazungumzo yalikuwapo huko nyuma,” alisema.

Aidha, alisema katika uchunguzi, kuna vitu viwili vinaweza kubainika: “Unaweza kukuta taratibu za kiutawala zilikiukwa au makosa ya jinai yalitendwa. Hatua inaendelea baada ya kuona nini kilifanyika. Hivyo bado tunaliangalia sababu watuhumiwa wote wameshahojiwa na vielelezo vyote tunavyo.

“Kama kuna hatua za kijinai tutapeleka jalada letu kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP), akibaini kuna makosa ya kijinai na yakithibitishwa tunakwenda mahakamani,” alikaririwa Mlowola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles