24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUTUMA WATAALAMU KUKAGUA NDEGE

NA NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM


SERIKALI imesema itatuma wataalamu kwenda kukagua ndege   ya Boeing 787 Dreamliner kabla haijaja nchini kwa ajili ya kuanza kutumika rasmi.

Hiyo ni  baada ya kuwapo   taarifa mbalimbali zinazodai  ndege hiyo haina viwango.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema utengenezaji wa ndege hufanywa kwa awamu na kwamba kila hatua wataalamu huwa wanakwenda kukagua.

“Nitafuatilia taarifa hizo lakini kwa kawaida huwa tunalipia kiasi fulani na kila hatua huwa tunaitwa kuikagua…lakini najua wataalamu watakwenda kuikagua,” alisema Profesa Mbarawa.

Hivi karibuni,  Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo), alisema   ndege hiyo ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens.

“Nimefanya utafiti kidogo na nimethibitisha kuwa tumenunua ndege zilizokataliwa hata na Rwanda rafiki zetu, kinachofuata ni kikubwa zaidi,” alisema Zitto.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Serikali iliweka maazimio ya kununua ndege nne kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuboresha safari za anga nchini.

Ndege mbili ndege mpya za Bombardier Q400 zilinunuliwa katika awamu ya kwanza, Septemba mwaka jana na Rais Dk. John Magufuli ndiye aliyezizindua.

Rais Dk. Magafuli alisema Serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 150  kuboresha usafari wa anga na kuleta ushindani wa biashara katika mataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles