22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

PROF. MAGHEMBE ASIFU  KUKUA SEKTA YA UTALII

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAMWAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amesema sekta ya utalii nchini inakua kwa kasi.
Amesema hiyo inatokana na mazingira ya mapokezi  wanayopata watalii   katika hoteli mbalimbali na sehemu nyingine zenye vivutio vya utalii.


Hayo aliyasema   Dar es Salaam jana baada ya kukabidhi vyeti vya kutambua hadhi za hoteli zilizopo na kuzipa madaraja mpaka nyota tano katika soko la utalii   nchini.


Alisema   mwaka jana watalii milioni 1.2 waliingia nchini Tanzania huku Kenya ikiwa ni milioni 1.3  na nchi nyingine za Afrika Mashariki zikiwa na watalii wadogo zaidi hivyo kuifanya Tanzania kuendelea kujivunia na kuboresha mazingira zaidi.


Alisema biashara ya hoteli inachangia pato la taifa kwa asilimia 25 hivyo ni muhimu katika kuongeza pato la Taifa kwa kuvuta watalii zaidi nchini.


Akigawa vyeti vyenye hadhi ya nyota tano aliitaja Serena kuwa na nyota tano na vigezo vilivyotumika.
Waziri alisema vimetumika vigezo vya usafi wa mazingira kwa kutotiririsha maji machafu ovyo na huduma nzuri.


Alizitaja hoteli nyingine zilizoshika namba nne kuwa ni   Ramada Hotel na Double Tree . Nyota tatu ni   Land Mark , Coral beach, Ramada ya Posta, Peninsula na Holday Inn.


Nyota tatu nyingine ni Saphire, Millenium Tower, Regency Park, Tiffany, Slip way, Tanzanite na Golden Tulip hotel.
Baadhi ya hoteli zenye nyota mbili ni   Shamool Hoteli ,City style Mbezi Garden .


 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama  vya Utalii Tanzania (TCT),  Abdulkadir Mohamed,  alisema sifa hizo zimezingatia viwango vya Afrika Mashariki.


Aliwataka wamiliki wa  hoteli kuendelea kutoa huduma bora zaidi na zaidi   kuvutia watalii zaidi.

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,215FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles