24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuimarisha mikakati ya kukabiliana na maafa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali imesema inaendelea kuweka mikakati madhubuti namna ya kujikinga na kukabiliana na maafa ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza na kuhatarisha usalama wa raia pamoja na kuharibu miundo mbinu.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya akifafanua jambo wakati wa semina kwa Kamati hiyo kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa Nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Balozi. Dk. Pindi Chana katika semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa nchini iliyoandaliwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

 “Hivi sasa Mheshimiwa Mwenyekiti nikuhakikishie elimu inayotolewa katika shule zetu  za Msingi Sekondari na  ngazi ya vyuo vikuu inalenga vijana wetu na jamii yetu  kujua Maafa kwa ujumla ili kujikinga wasipate madhara,” amesema Pindi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Charles Msangi akiwasilisha Dhana na Mfumo wa Usimamizi  wa Maafa Nchini katika semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Aidha, amebainisha kwamba utafiti unaofanywa na watalaamu mbalimbali kuhusu Mazingira na Maafa utumike vyema kama moja ya njia ya kukabili maafa ya asili na yale yatokanayo na shughuli za kibinadamu. Utafiti hutoa mwanya wa kujua hatua sahihi za kuchukua kabla ya majanga kutokea na baada ya kutokea.

Wakti huo huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya alifafanua kwamba muswada wa sheria ya Maafa utasaidia kuondoa changamoto zilizobainika kutokana na sheria ya zamani na wahusika kufahamu majukumu yao ili kuepusha muingiliano wa majukumu wakati wa utekelezaji wa shughuli zote za Maafa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Dk. Joseph Mhagama akieleza jambo wakati wa semina kwa Kamati hiyo kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa Nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Nae Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Najma Giga alishauri Mfuko wa Maafa kutengewa bajeti yake itakayosaidia kutatua changamoto zinazotokana na Maafa badala ya kusubiri hadi yatokee na kuanza kutafuta wadau kwa ajili ya kutoa huduma.

“Tunaelewa waziwazi kuna Maafa ya kimaumbile ambayo huwenda yakatokea kila mwaka  kutokana na mvua za masika  au mabadiliko ya tabianchi kwenye fukwe zetu za bahari tunajua kabisa kila mwaka mabadiliko ya tabia nchi yanapotokea shemu ya ardhi inaliwa lakini ikitokea Maafa ndio tunaanza kupambana kutafuta wadau. Mfuko unaanza kutuna kwanini sasa serikali isione utaratibu utakaowekwa maalumu kwa hao hao watu wanaotusaidia,” ameeleza Makamu Mwenyekiti huyo.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakichangia hoja katika semina hiyo kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi  wa Maafa Nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma

Akihitimisha wasilisho la dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa katika semina hiyo Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Charles Msangi alisema Muswada wa sheria imezingatia uwajibikaji wa wadau wote kwani ulifanyika utafiti ambao uliangalia majukumu ya kila mdau .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles