24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuandaa rasmu ya kulinda maeneo ya kilimo nchini

Na Upendo Mosha, Arusha

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, amesema serikali ipo katika mchakato wa kuandaa rasimu ya sheria ya kulinda maeneo ya kilimo nchini hatu ambayo itasaidia kuzuia uvamizi na kuhatisha uhai wa kilimo cha baadhi ya mazao.

Mkenda ameyasema hayo jana jijini Arusha, wakati akizungumza na wawekezaji wa kilimo kutoka nchi za ulaya, katika mkutano iliyolenga kujadiliana juu ya changamoto wanazokutananazo wawekezaji hao.

Amesema ipo haja ya maeneo ya kilimo kulindwa kwa kutumia sheria na kwamba wizara ya kilimo ipo katika mchakato wa kuandaa rasimu hiyo ya mswaada wa sheria itakayobeba jukumu la kulinda maeneo ya kilimo na kuwa endelevu.

“Tayari serikali imeshaandaa rasimu ya sheria ya kilimo ambapo pamoja na mambo mengine italinda maeneo ya aridhi ambayo yametegwa kwaajili ya kilimo yasifanyiwe maendeleo…mfano maeneo ya Dodoma Mjini pale ndo ardhi inafaa kwaajili ya kilimo cha zabibu sio sehemu yote ya Dodoma lazima tuilinde,” amesema Prof. Mkenda.

“Tukiacha ardhi yote ikichukuliwa kilimo cha zabibu na mazao mengine kitaisha kabisa…lakini pia serikali imekubali kutoa ardhi kwaajili ya kilimo na tunaongeza Kasi ya kuwa na mpango mzuri wa ardhi kwaajili ya kilimo”alisema

Mbali na hilo waziri mkenda alipiga marufu upandishwaji holela wa bei ya sukari unaofanywa na baadhi ya wafanyabishara na kwamba serikali ikiagiza zaidi ya tani 50,000.

“Serikali ikiagiza tanio 50,000 za sukari upugufu wa sukari hamna na isitoshe viwanda vyetu vya ndani tayari vimeshaanza uzalishaji…niwaonye wafanyabishara waache kuoandisha bei ya sukari,” amesema Prof. Mkenda.

Katika hatua nyingine Prof. Mkenda amewataka wawekezaji katika sekta ya kilimo, kuhakikisha wanatumia fursa za kuzalisha aina bora za mbegu za mimea inayozalisha mafuta jambo ambalo litasaidia serikali kuacha kuagiza bidhaa hiyo nje ya nchi.

“Kwa sasa mbali na kuwa na upungufu wa mafuta ya kula nchini pia mbegu hatuna nyingi tunaagiza nje naombeni mtumie fursa hii mzalishe mbegu ili tujitosheleze ndani ya nchi na ikitokea tunaagiza tuagize chache,” amesema.

Rory Nightingale mwekezaji katika sekta ya kilimo, ambaye amesema, hatua ya serikali ya kukutana na wawekezaji imetoa fursa kwao kusema changamoto zinazo wakabili na kwamba wanaimani zitatuliwa.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya kilimo cha matunda na Mboga (TAHA), Jacqueline Mkindi, amesema watahakikisha wanashirikiana na serikali katika kuimarisha sekta hiyo.

“Tutashirikiana na serikali maana bajeti iliyoletwa na wizara ya Fedha imeonyesha Mwanga kwenye sekta ya kilimo sisi ni miongoni mwa sekta zilizopendelewa,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles