29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Majaliwa ahimiza Watanzania kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi

Na Ramadhan Hassani, Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kuweka utaratibu wa
kufanya mazoezi huku akiziagiza Halmashauri kupitia Maafisa Michezo
na Utamaduni kuandaa vikundi na viwanja kwa ajili ya kufanya mazoezi.

Akizungumza leo, June 12,2021 katika Bonanza liloandaliwa na Benki ya
CRDB, katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa
amezitaka Halmashauri ziandae viwanja kwa ajili ya kufanya mazoezi.

“Halmashauri ziandae viwanja kwa ajili ya kufanya mazoezi tuanze
kuviandaa kama havipo Maafisa Utamaduni na Michezo ni lazima waunde
vikundi. Nitoe wito tuendelee kuunda vikindi vya mazoezi inakuwa rahisi
kuhamasishana inatusaidia kushiriki Michezo,”amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amewataka watanzania kuweka utaratibu wa kufanya
mazoezi asubuhi ama jioni lengo likiwa ni kuiweka miili vizuri.

“Lazima tuendelee tuhakikishe tunafanya mazoezi wakati wote uwanja huu
Jamhuri upo wazi tunaona vikindi na Wabunge huu uwanja ni wetu sote
tufanye mazoezi  jioni au asubuhi,” amesema Majaliwa.

Majaliwa ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa bonanza hilo ambapo
amesema lengo la bonanza hilo ni kuwaleta pamoja watanzania kwa ajili
ya kufanya mazoezi,kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan  za
kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi pamoja na kupata burudani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela amesema  lengo kuu la kuandaa bonanza hilo ni kuisogeza benki
hiyo karibu na Serikali, Bunge na Wizara, ili kupata nafasi ya
kusikiliza mahitaji yaliyopo na kujua namna gani benki hiyo inaweza
shiriki kikamilifu katika mipango ya maendeleo ya nchi.

“Miaka ya nyuma tulikuwa tukifanya bonanza hili na Bunge, mwaka huu
tumeshirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kushirikisha Wizara zote.
Malengo yetu mwakani ni kuhusisha muhimili mwengine wa Serikali
kwamaana ya Mahakama,” aliongezea Nsekela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles