25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Jamii ijengewe uelewa kuhusu teknolojia ya mionzi- Prof. Ndalichako

Na Mohammed Ulongo, Dar es Salaam

Waziri wa Elimu, Sayanasi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, amesema ni muhimu kwa jamii kuwa na uelewa kuhusu teknolojia ya Nyuklia kwani ni teknolojia mtambuka kwakua inatumika katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya Afya, Kilimo Ujenzi, Maji , Viwanda, Barabara na Madini huku katika sekta ya afya ikitumika kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Mkurgenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala, akizungumza wakati wa Mafunzo Kitaifa kwa Wahariri na Waandishi wa Habari juu ya uelewa na udhibiti na Matumizi Salama ya Mionzi nchini.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo Juni 12, 2021 wakati akifungua mafunzo ya Kitaifa kwa Wahariri na Waandishi wa Habari juu ya uelewa na udhibiti na matumizi salama ya mionzi nchini yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Prof. Ndalichako amesema kupitia mafunzo hayo yataweza kuwajengea uelewa wahariri na waandishi wa habari kuhusu shughuli za Atomic na kuondoa dhana hasi iliyojengeka kwenye jamii.

“Kufuatia mafunzo haya tunaimani kwamba itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza madhara kwa wananchi na mazingira kupitia matumizi ya mionzi isiyo salama kwakuwa waandishi wa habari na wahariri ni kiungo muhimu katika jamii kufikisha taarifa na kuijengea jamii uelewa kuhusu jambo fulani,” amesema Prof. Ndalichako.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala amesema kuwa mafunzo hayo yanaweza kusaidia kuondoa zana potofu katika jamii kwani kumekuwa na uelewa hafifu kuhusu matumizi ya mionzi.

Mkuu wa Ofisi ya Kanda ya Dar es Salaam Tume ya Unguvu za Atomiki (TAEC), Dk. Wilbroard Muhogora (kushoto) akiwa na Mtafiti Mwandamizi Sayansi ya Nyukilia, Alex Muhulo.

Amefafanua kuwa mafunzo hayo ni endelevu na yatawafikia makundi mbalimbali katika jamii lengo likiwa jamii nzima ielewe matumizi sahihi ya mionzi kwa manufaa ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. William Anangisye amesema Chuo hicho ni mdau mkubwa wa masuala ya nguvu za atomiki ikiwemo chuo hicho kuwa na kozi maalumu kuhusu masuala ya nguvu za atomiki.

“Kwa mwaka wa masomo 2020/2021 Chuo kikuu cha Dar es Salaam kimedahili wanafunzi 60 wanaosoma kozi inayohusiana na nguvu za atomiki huku kukiwepo na wanafunzi 7 wanaosomea shahada ya umahiri kuhusu masuala ya nguvu za atomiki,” amesema Prof. Anangisye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles