23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Serengeti Boys kutua leo Sauzi

Serengeti-BoysNa MARTIN MAZUGWA-DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, inatarajia kutua leo nchini Afrika Kusini (Sauzi) kupambana na vijana wenzao wa nchi hiyo katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Kombe la  Mataifa Afrika kwa vijana utakaochezwa Agosti 6 mwaka huu.

Kikosi cha Serengeti Boys kinatua Afrika Kusini kikitokea Madagascar kilikoweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo huo ikiwa ni wiki chache tangu waitoe Shelisheli katika hatua ya awali ya kufuzu kwa matokeo ya jumla mabao 9-0

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema kwamba licha ya kufuzu kwa ushindi mnono, lakini walimu wameendelea kuimarisha safu ya ushambuliaji ili kuongeza makali zaidi hasa wanapokutana na timu ngumu kama ya Afrika Kusini.

“Mara baada ya kutoa sare na kupoteza  sana nafasi kwenye michezo ya kirafiki, mwalimu anaendelea kutoa mafunzo katika nafasi ya umaliziaji,” alisema.

Alisema kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi baada ya kupata sare katika mchezo wake wa kirafiki wa kujipima nguvu  na timu ya Taifa ya vijana ya Madagascar.

Alfred alisema mpaka sasa kikosi hicho hakina majeruhi na anaamini kitafanya vizuri katika mchezo ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles