23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Ajib amkosha Omog

Ibrahim-AjibNa THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIWANGO cha mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib, kimeendelea kumkosha kocha wa timu hiyo, Mcameroon Joseph Omog, wakati miamba hiyo ya Msimbazi ikiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Juzi Ajib alifunga mabao mawili na kuisaidia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro na kufikisha jumla ya mabao matano kwenye mechi tatu za kirafiki ambazo miamba hiyo ya Msimbazi imecheza hadi sasa.

Kasi hiyo ya Ajib ya kucheka na nyavu inaonekana kumkuna Omog kiasi cha kumfanya kocha huyo kuchelewa kusajili straika wa kimataifa kutokana na kile kinachoonekana kuridhishwa na kiwango cha mshindi huyo wa bao bora la mwaka katika msimu uliopita.

Hadi sasa Simba imecheza mechi tatu za kirafiki katika kambi yake ya Morogoro na kushinda zote ambapo mbali na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Burkina Faso, miamba hiyo ya Msimbazi pia ilishinda kwa mabao 6-0 mchezo wake dhidi ya Polisi Morogoro na mabao 2-0 dhidi ya Moro Kids.

Matokeo hayo ya Simba kwenye mechi zake za kirafiki mkoani Morogoro yameanza kurudisha matumaini kwa mashabiki wa miamba hiyo ya Msimbazi baada ya kufanya vibaya msimu uliopita.

Kikosi hicho ambacho kimeweka kambi kwenye Chuo cha Biblia mkoani Morogoro, kinatarajia kucheza dhidi ya Interclube ya Angola Agosti 8, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo maalumu wa tamasha la klabu hiyo maarufu kama ‘Simba day’.

Interclub wanatarajia kuwasili nchini Agosti 6 kabla ya mchezo huo maalumu utakaotumika kutambulisha kikosi kipya cha Wekundu wa Msimbazi na benchi la ufundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles