23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Serena kuitafuta rekodi ya 23 US Open

Serena Williams
Serena Williams

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA wa mchezo wa tenisi nchini Marekani, Serena Williams, anatarajia kuweka rekodi ya 23 katika michuano mikubwa ya Grand Slam katika US Open.

Nyota huyo alishindwa kushiriki michuano ya Cincinnati wiki iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya bega baada ya kurudi katika michuano ya Olimpiki nchini Brazil.

Mbali na kusumbuliwa na maumivu hayo, kocha wake, Patrick Mouratoglou, amedai kuwa nyota huyo bado bega lake alijawa sawa kwa asilimia 100, lakini anaweza kucheza michuano hii ya US Open na kuweka historia.

Bingwa huyo namba moja kwa ubora duniani kwa upande wa wanawake, anatarajia kushuka dimbani leo dhidi ya mpinzani wake kutoka nchini Urusi, Ekaterina Makarova, huku kocha huyo akidai kuwa maumivu ya Serena si makubwa na hayawezi kumsumbua.

“Maumivu ya Serena ndani ya siku hizi chache yametulia, ni wazi kwamba bega hilo halijakamilika kwa asilimia 100, lakini bado kidogo sana kupona, hivyo kwa sasa yupo katika hali zuri ya kupambana.

“Alikwenda kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil lakini bega lilimfanya ashindwe kufanya vizuri, nguvu zake anazimalizia kwenye michuano hii ya US Open,” alisema Mouratoglou

Serena alifanikiwa kufanya vizuri katika michuano ya Wimbledon mwezi uliopita na kutwaa taji hilo alipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya Olimpiki lakini aliyaaga mashindano hayo mapema.

Tangu atolewe kwenye michuano hiyo ya Olimpiki, hadi sasa hajafanikiwa kushuka dimbani, lakini leo ataonesha uwezo wake katika US Open.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles