30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti wa kijiji achapwa viboko mkutanoni

fimbo-640x336

Mwenyekiti wa Kijiji cha  Simike  Kata  ya Lufingo  wilayani Rungwe,  Efram  Kapondany’a amechapwa  bakora  mbele  ya  mkutano  wa  hadhara   baada ya  kuwasilisha Sh 10,000 tu  akidai  ndiyo mapato  ya  mwaka  ya  masoko  na magulio ya kijiji.

Inaelezwa kuwa   mwenyekiti  huyo alikuwa amegoma  kuwasomea   wanakijiji mapato  na  matumizi ya kijiji kwa  zaidi  ya  mwaka  mmoja, hali iliyowakasirisha wananchi hao na kuamua kumcharaza viboko mkutanoni.

Kwa mujibu wa wananchi hao,   Mwenyekiti  huyo  na Ofisa Mtendaji  wa  Kijiji hicho, Babelina  Mlaghala  walichakachua mali  za  kijiji pia Kupiga chenga kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji  hali iliyosababisha wachukue hatua  madhubuti ya   kumcharaza bakora mwenyekiti huyo kama  fundisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles