23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Waziri wa Habari afungia Redio mbili

Nape Nnauye
Nape Nnauye

Serikali imevifungia kwa muda usiojulikana vituo vya redio vya Magic FM cha jijini Dar es Salaam na Redio Five cha jijini Arusha kwa madai ya kukiuka maadili, kanuni za utangazaji na kudaiwa kuleta maudhui ya uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wa vituo hivyo unakiuka masharti ya kanuni zilizopo.

Alisema kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 28 (1) cha sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2013 ameamua kuvifungia vituo hivyo hadi hapo Kamati ya Maudhui itakapokutana na kuwasikiliza kwa kina zaidi na kushauri hatua zaidi za kuchukua kwa mujibu wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles