26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Schmeichel: Van Gaal hawezi kuipa United ubingwa

Champs League SF Peter SchmeichelMANCHESTER, ENGLAND

MLINDA mlango wa zamani wa klabu ya Manchester United, Peter Schmeichel, amedai kwamba klabu hiyo haiwezi kuchukua ubingwa wa ligi kwa kutumia mifumo ya kocha wao, Van Gaal.

Schmeichel alitoa mchango mkubwa katika klabu hiyo akiwa chini ya kocha Aleix Ferguson, tangu mwaka 1991-1999, ambapo aliipa mataji mbalimbali na kuweka jina lake katika kumbukumbu ya wachezaji wa klabu hiyo ambao wametoa mchango mkubwa.

Hata hivyo, nyota huyo hana imani na mifumo ambayo anatumia kocha huyo kwa wachezaji wake kwa ajili ya kutafuta ubingwa msimu huu, hivyo amedai kwamba haiwezekani klabu hiyo kutwaa ubingwa.

Juzi klabu hiyo ilishuka dimbani kwenye Uwanja wa Anfield kupambana na wenyeji Liverpool, ambapo United ikafanikiwa kuondoka na alama tatu ugenini huku bao hilo la ushindi likifungwa na Wayne Rooney.

“Sina uhakika kama United inaweza kuchukua ubingwa, sina uhakika kama timu hiyo imekamilika, sina uhakika kama timu hiyo inafurahia jinsi inavyocheza.

“Katika mchezo wa juzi ilifanikiwa kupata pointi tatu dhidi ya Liverpool hii ilikuwa ni bahati kwao hasa kutokana na uwezo ambao aliuonesha katika mchezo huo na naweza kusema yeye ndio kila kitu kwa United.

“Kama uchezaji wenyewe ndio huu Manchester United haiwezi kuchukua ubingwa wa ligi kutokana na mifumo ambayo Van Gaal anaitumia, maana kila mchezo ambao anashinda inakuwa ni bahati,” alisema Schmeichel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles