27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Jada awatupia lawama waandaaji wa tuzo za Oscar

JadaNEW YORK, MAREKANI

MKE wa nguli wa filamu nchini Marekani, Will Smith, Jada Pinket, amewatupia lawama waandaaji wa tuzo za Oscar kwa kutowahusisha wasanii weusi.

Tayari orodha ya wasanii ambao wanatakiwa kuwania tuzo hizo wametajwa tangu Alhamisi ya wiki iliyopita, lakini cha kushangaza ni kwamba hakuna majina ya wasanii weusi.

Katika orodha hiyo wasanii ambao wametajwa ni wale wenye ngozi nyeupe huku ngozi nyeusi wakiwa katika nafasi ya kugawa tuzo hizo na sio kuwania.

“Ni kitendo cha ajabu kwa waandaaji wa tuzo hizo wanaonesha wazi kuna ubaguzi wa rangi, haiwezekani wasitambue mchango wa wasanii weusi ila wanatambua uwezo wao haina maana yoyote.

“Wanatakiwa kuonesha heshima kwa wasanii wa aina zote bila kujali rangi yao, lakini kwa hali hii ni wazi kwamba kuna wasanii ambao watakuwa tayari kujitoa kwa namna moja ama nyingine,” alisema Jada.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Februari 28 mwaka huu nchini Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles