23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki wamzomea Lil Wayne

2012 iHeartRadio Music Festival - Day 1 - ShowMILAN, ITALIA

RAPA kutoka kundi la Young Money, Lil Wayne, alijikuta akiwarushia kipaza sauti kwa hasira mashabiki wake baada ya kuona anazomewa mjini Milan.

Msanii huyo alikuwa mjini Milan nchini Italia mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Philipp Plein, lakini mambo yalionekana kuwa tofauti baada ya msanii huyo kupanda jukwaani ambapo mashabiki hawakuonesha ushirikiano zaidi ya kumzomea.

Lil Wayne aliwataka mashabiki wake kuinua mikono juu, lakini walikuwa kimya na kuanza kumzomea bila sababu za msingi na ndipo msanii huyo akaamua kuwarushia kipaza sauti huku akisikika kusema kwamba ‘hivi ndivyo mlivyotaka nifanye?

Kutokana na hali hiyo, Lil Wayne aliamua kushuka jukwaani huku akionekana anaongea maneno ambayo yalikuwa hayasikiki kwa mashabiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles