24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Shindano la kusaka wasomi wenye vipaji laja

NA GEORGE KAYALA

KAMPUNI ya Afrika Nasaha Production ya nchini Kenya, inatarajia kuanzisha shindano la kusaka waimbaji wenye vipaji kutoka vyuo mbalimbali vya elimu nchini na washindi watafadhiliwa ada na kurekodiwa nyimbo zao katika mfumo wa audio na video.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkurungenzi wa kampuni hiyo, Francis Mwanzi, alisema kuwa shindano hilo linaitwa ‘Dream Come True’ na sasa yupo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kuomba kibali cha kuendesha shughuli hiyo ambayo itakuwa msaada kwa wasomi wenye ndoto ya sanaa maishani mwao.

“Nipo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuomba kibali cha shindano la Dream Come True na mara mambo yatakapokuwa tayari Watanzania watajulishwa siku ya kuanza kwa shindano hilo.

“Shindano hilo litakuwa linarushwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga ili kuweza kuwafikia Watanzania wengi, ninaamini litapokelewa vizuri kutokana na kile ambacho tumepanga kukifanya,” alisema Mwanzi.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa amefanikiwa kuendesha kwa mafanikio shindano hilo nchini Kenya na sasa ni mwaka wa 10 na huwa linafanyika mara tatu kwa mwaka, Aprili, Agosti na Desemba na kuwataka Watanzania wamwombee ili afanikishe jambo hilo hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles