26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Klopp adai hawakustahili kufungwa na United

KloppLIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amewashangaa wachezaji wake kwa kupoteza nafasi nyingi katika mchezo dhidi ya Manchester United na kudai kwamba hawakuwa na sababu ya kuupoteza mchezo huo.

Liverpool ilikubali kichapo cha bao 1-0 kwenye uwanja wa nyumbani Anfield, lakini Klopp anawashangaa wachezaji wake kushindwa kutumia nafasi nyingi walizozipata dhidi ya wapinzani wake.

“Ni wazi kwamba tulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, tulipata nafasi zaidi ya tano lakini tulishindwa kuzitumia wakati wapinzani wetu walipata chache na walifanikiwa kuitumia moja.

“Bila shaka mlinda mlango wao, David De Gea alitoa mchango mkubwa wa kulilinda lango lao na aliwapa wakati mgumu washambuliaji wangu kwa kuwa alikuwa anaokoa mipira mingi ya hatari.

“Lakini kwa matokeo haya yamenifanya nijisikie vibaya hasa katika uwanja wa nyumbani wakati tulikuwa na nafasi kubwa ya ushindi,” alisema Klopp.

Hata hivyo, kocha huyo amedai kwamba kwa sasa anajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Norwich mwishoni mwa wiki hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles