27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

SBL YAANZA KUUZA BIA KENYA

Na MWANDISHI WETU


KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imeanza kuuza bidhaa zake nchini Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha, alisema wameanza kupeleka bidhaa zao katika soko la kikanda, ambapo shehena ya kwanza ya bia  inayoitwa Allsopps ilisafirishwa kwenda nchini Kenya wiki iliyopita.

Wanyancha alisema: “Hii ni hatua nyingine ya kufurahisha katika kampuni yetu na kwa bidhaa zetu. Kumudu kupenyeza bidhaa zetu ndani ya soko la Kenya kunadhihirisha ubora wake hivyo kuzifanya zikubalike ndani na nje ya nchi.”

Alisema SBL inaangalia uwezekano wa kupanua mauzo ya biashara katika masoko mengine ya kikanda, hatua ambayo iko katika mkondo wa kuhamasisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kada nyingine za kiuchumi kuongeza biashara yake ya kuvuka mpaka ndani ya ukanda huo.

Alitaja aina nyingine ya bidhaa wanazozalisha na kutambulika kimataifa kuwa ni Pilsner Lager, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness Stout, Uhuru, The Kick pamoja na bidhaa kuu ya Serengeti Premium Lager-ambayo peke yake imeshajizolea medali kumi zinazotambuliwa kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles