29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

Samu wa Ukweli kuzikwa kesho kijijini kwao Kiwangwa mkoa wa Pwani

Na LULU RINGO


MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Salim Mohamed maarufu Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua tangu Jumamosi iliyopita.

Kabla ya kifo chake alipohojiwa na rafiki zake pamoja na prodyuza wake, Steve nini kilichokuwa kikimsumbua jibu lake lilikuwa ni kwamba alikuwa akiumwa ukimwi wa kulogwa maneno ambayo alikuwa akipenda kuyaeleza mara kwa mara kipindi cha uhai wake.
“Alianza kuzidiwa toka jumamosi tulipomuhoji alisema anaumwa ukimwi lakini sio ukimwi wa kawaida bali ni wa kulogwa,” alisema prodyuza wake, Steve.
Steve Alifafanua zaidi kwamba kabla ya umauti kumkuta msanii huyo aliyekuwa studio akiandaa wimbo wake mpya lakini kabla wimbo huo haujakamilika alianza kulalamika maumivu ya tumbo na baada ya muda aliishiwa nguvu wakamkimbiza ‘pharmacy’ moja iliyopo mabibo lakini walishauriwa wamkimbize hospitali ya Palestina ambapo umauti ulimkuta.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na utasafirishwa leo jioni kijijini kwao kiwangwa Bagamoyo mkoa wa Pwani ambapo maziko yatafanyika kesho mchana.
Msanii huyo ameacha mke na watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wakiume. Mtanzania Digital tunamuombea roho yake ipumzike kwa amani, Amen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles