22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

JINSI YA KUTENGENEZA ACHARI YA EMBE

Mahitaji

  1. Embe mbichi kubwa 1
  2. Chumvi vijiko 2 vya chai
  3. Pilipili ya unga vijiko 2 vya chai.
  4. Mdalasini kijiko 1 cha chai.
  5. Uwatu usiosagwa 1/2 kijiko cha chai
  6. Paprika1/2 kijiko cha chai au tandoor masala
  7. Chupa ya kuhifadhia
  8. Mafuta ya kupikia vijiko 5 vya chakula

 

Jinsi ya kuandaa
Katakata vipande vidogo vidogo vya embe

Weka chumvi katika sufuria, kaanga hadi iwe rangi ya kahawia (usiweke maji). Acha ipoe,

pasha mafuta moto halafu acha yapoe kidogo, baada ya hapo weka paprika,

pilipili, binzari na viungo vyote, changanya vizuri.

Weka chumvi na maembe changanya vizuri.

Funika mchanganyiko, acha ikae usiku kucha ili embe ilainike.

Siku ya pili tayari kwa kutumia, unatakiwa kuiweka juani ili embe ilainike vizuri zaidi. Lakini ni hiari, si lazima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,208FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles