25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Samia: CDA msifanye kazi kwa mazoea

samia-suluhuNa SARAH MOSES, DODOMA

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameitaka Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) kubadilika kiutendaji na kuepuka kufanya kazi kimazoea ili kuendana na kasi ya Rais Dk. John Magufuli.

Pia amewaagiza viongozi wa Serikali mjini hapa kuiangalia CDA kwa umakini wa hali ya juu ili mamlaka hiyo ifanye kazi kwa mafanikio zaidi.

Samia aliyasema hayo mjini hapa juzi kwenye ukumbi wa hazina alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya wakazi wa Mji wa Dodoma.

“CDA imekuwa ikilalamikiwa na wananchi na imekuwa ikifanya kazi kwa mazoea, hali inayosababisha kutokuwapo kwa mawasiliano mazuri baina yao, manispaa pamoja na wananchi.

“Kwa hiyo, lazima mambo hayo myaondoe ili kazi zifanyike kwa kufuata sheria na utaratibu ili yasiwepo malalamiko,” alisema Samia.

Samia ambaye ana ziara ya siku nne mjini hapa, alitembelea pia dampo lililopo eneo la Chidaya na pia alikagua ujenzi wa jengo la ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kuzungumza na makundi mbalimbali ya wakazi wa mjini hapa.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais amesema Dodoma kuna mapato mengi, lakini anashangaa kuona manispaa inaingiza mapato kidogo.

Kutokana na hali hiyo, alimtaka mkurugenzi wa manispaa hiyo kuhakikisha mapato hayo yanaongezeka baada ya kukusanywa kama inavyotakiwa.

“Kusanyeni mapato kama inavyotakiwa na kama mnakusanya mengi halafu watu fulani wanakula, hakikisheni mnaziba mianya hiyo haraka sana,” alisema.

Pamoja na hayo, Makamu wa Rais alisema hajaridhishwa na mazingira ya Mji wa Dodoma, hivyo alimwagiza Mkuu wa Mkoa huo, Jordan Rugimbana, na wakuu wa wilaya zote za mkoani hapa kuhakikisha wanapanda miti kama ilivyokuwa jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles