27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wafugaji waendelea na mgomo wao

wafugaNa RAMADHAN LIBENANGA, MOROGORO

WAFUGAJI mkoani Morogoro, wameendelea  kugoma kuchinja ng’ombe ili kuishinikiza Serikali isitishe upigaji chapa mifugo yao.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wafugaji hao walisema wamelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na uamuzi huo wa Serikali.

Kiongozi  wa  kundi  la  wafugaji hao, Mfalme  ole Kelei, alisema tamko la Serikali la kukataza  mifugo isiyopigwa chapa isiuzwe mnadani, ni dalili za unyanyasaji ambao hawako tayari kuukubali.

“Inawezekana lengo la Serikali ni zuri, lakini walitakiwa kutuelimisha kwanza na si kutoa amri pasipo kutushirikisha wafugaji.

“Kwa hiyo, hatutakubali kuchinja mifugo yetu hadi hapo watakapokuja na kutuelewesha faida za chapa hizo na madhara ya kutopiga chapa,” alisema ole Kelei.

“Narudia tena, tunamwomba waziri  mwenye dhamana ya mifugo aje atutolee  ufafanuzi wa suala hilo, vinginevyo hatutabadili msimamo wetu,” alisema ole Kelei.

Mgomo  wa  wafugaji  kukataa  kuchinja  ng’ombe ulianza wiki iliyopita, baada ya wafugaji hao kugoma kutekeleza agilo la Serikali la kupiga chapa mifugo yao.

Kutokana na hali hiyo, wafanyabiashara wanaouza nyama mjini hapa wameanza kupandisha bei ya bidhaa hiyo, jambo linalowaumiza watu wenye kipato kidogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles