27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

ATCL yatoa ofa ya safari za Mwanza

atcl-yatoa-ofa-ya-safari-za-mwanzaNa Daudi Manongi-MAELEZO

KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) imetoa ofa ya mwezi mmoja kwa abiria watakaosafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kwa kulipa nauli ya Sh 160,000  kwa safari moja.

Akizungumza   Dar es Salaam jana, Kaimu Ofisa Mawasiliano wa ATCL, Lily Fungamtama alisema ndege za kampuni hiyo zimeanza kutoa huduma kuanzia Oktoba 15, mwaka huu.

“Safari hizo zilianza kwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kwenda  Comoro na hapa nchini zipo katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Kigoma,” alisema Lily.

Alisema yalianza   mazoezi ya vitendo kwa marubani na wafanyakazi wa ndani ya ndege na hatimaye zilianza safari za biashara ya kusafirisha abiria Oktoba 15, mwaka huu.

Alisema ATCL imeboresha huduma zake kwa kiasi kikubwa kwa kuwapatia wateja wake ofa ya kubeba kilo 20 za mizigo na kilo saba za mzigo wa mkononi bure   na kutoa vinywaji na ubadilishaji wa tiketi ni bure ndani ya mwezi.

Pamoja na hali hiyo alitoa ufafanuzi kwa kile kilichodaiwa kukwama kwa safari na kusema hakuna na ratiba inakwenda kama ilivyopangwa.

ATCL kwa sasa ina ndege tatu zikiwamo mbili aina ya Dash8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na Dash8-Q300 moja yenye uwezo wa kubeba  abiria 50.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles