24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Jinsi mabilioni ya NICOL yalivyochotwa

moshaNA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RIPOTI ya Kampuni ya Uwekezaji ya NICOL imeanika namna Sh bilioni nane zilivyochotwa na kugawanywa kwa uongozi wa muda wa kampuni hiyo.

Menejimenti hiyo ya muda ya NICOL inaongozwa na Gideon Kaunda na Adam Wamuza ambao wanalalamikiwa na wanahisa kwamba hawako kwa halali.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo ilitolewa kwa wanahisa waliofika kwenye mkutano uliozuiliwa na polisi mwishoni mwa wiki kwa sababu za  usalama.

Wakati uongozi wa muda NICOL ukichota mabilioni hayo ya fedha kwa muda mfupi, inadaiwa kuwa kwa miaka zaidi ya 10 kabla ya uongozi wa muda kuingia, Bodi ya Wakurugenzi ikiongozwa na Felix Mosha ilitumia Sh milioni 10 kwa mikutano ya bodi na gharama nyingine

“Kabla ya kujiingiza kwenye matarakimu ya fedha zilizotolewa benki, ni muhimu kujibu swali kama wanaojiita menejimenti ya muda.

“Nicol inayoongozwa na Dk. Gideon Kaunda na Adam Wamunza wamepata wapi uhalali wa kutoa fedha za wanahisa benki?” ilihoji ripoti hiyo.

Hata hivyo   ripoti hiyo iliyoandaliwa na bodi ya wakurugenzi ya NICOL inayoongozwa na Felix Mosha, inaonyesha malipo yaliyofanyika yana utata mkubwa ambao wanahisa walipaswa kujadili na kutoa uamuzi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, fedha zilizolipwa kwa wanaojiita menejimenti ya muda zilifikia Sh milioni 184.9 ambazo hazikueleza yalikuwa malipo ya nini

Fedha za mshahara zilizotolewa kwa kiwango cha Sh milioni 12 kila mwezi kwa miezi 16, zilifikia Sh milioni 192 lakini hazioneshi zililipwa kwa nani.

Ripoti hiyo inaonyesha fedha zilizotolewa kwa ajili ya mishahara na zilitolewa kwa mafungu makubwa.

Mbali na hilo ripoti hiyo ilitaja fedha zilizolipwa watu binafsi kuwa ni Sh 695.16 na katika malipo hayo yote, ni   Sh milioni 22.98 tu zinazoonyeshwa kuwa zilikuwa ni marejesho ya gharama za matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles