26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

SAMATTA TUKUTANE ENGLAND MSIMU UJAO

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


samataNI wazi kuna uwezekano mdogo kwa Mtanzania, Mbwana Samatta kuondoka katika klabu yake ya K.R.C Genk ya Ubelgiji na kujiunga na klabu nyingine zinazocheza Ligi Kuu England katika kipindi hiki cha usajili mdogo Barani Ulaya.

Kucheza Ligi Kuu England ni ndoto ya kila mchezaji, kutokana na ubora wa ligi hiyo inayodaiwa kupendwa na mashabiki wengi wa soka duniani.

Asilimia 70 ya mashabiki wa soka ulimwenguni, wanadaiwa kufuatilia ligi hiyo ambapo wengi wao wanatoka Afrika.

Samatta alijiunga na Genk Januari mwaka jana kwa Euro milioni 2.5, ambazo sawa na Shilingi bilioni 5 za Tanzania, bado amebakiwa na mkataba wa  miaka mitatu kati ya minne na nusu aliyosaini kucheza katika klabu hiyo.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) amecheza michezo 20 na kufunga mabao matano katika Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Samatta kwa sasa hana kiwango kizuri tangu kuanza kwa duru la pili la ligi hiyo, ambapo Genk kwa sasa ipo nafasi ya tisa ikiwa na pointi 28, huku ikielezwa kuwa ndio nafasi mbaya kuwahi kutokea katika timu hiyo.

Kutokana na  mwenendo huo mbovu uongozi wa klabu hiyo, ulimtimua kocha wake, Peter Maes.

Maes  ndio kocha ambaye kwa mara kwanza, alipendekeza kusajiliwa kwa Samatta katika timu hiyo, hivyo kuondoka kwake huenda kukawa na  tafsiri kubwa, kuhusu maisha ya Samatta ndani ya Genk.

Kwa upande mwingine kutupiwa virago kwa kocha huyo, kunaweza kuwa moja ya sababu itakayomsukuma Samatta kutamani kuondoka Genk.

Kwani kwa sasa hana uhakika kama ataweza kumshawishi kocha mpya, hata hivyo wazo la kuondoka halitakuwa rahisi kwa sasa kutokana na kuondoka kwa Wilfred Ndidi, aliyetua timu ya Leicester City ya England.

Ndidi ametua Leicester City kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15, baada ya kibali cha kufanya kazi Uingereza kuidhinishwa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria, alifaulu vipimo vya afya kujiunga na Leicester mapema, wiki iliyopita na alikubari vigezo na masharti kusaini mkataba wa miaka mitano.

Uchezaji wa Ndindi umefananishwa na ule wa nyota wa zamani wa Leicester City, N’Golo Kante, tayari kucheza mechi za wikiendi za Kombe la FA dhidi ya Everton.

Nyota huyo alianza kufanya mazoezi na wachezaji, wenzake wa klabu yake mpya kwa mara ya kwanza Alhamisi iliyopita.

Kocha wa timu hiyo Claudio Ranieri anasema: “Ndindi ni mchezaji mwenye mvuto na mwenye mustakabali ngavu.

Ni mrefu na anaruka vizuri sana kwa ajili ya mipira ya kichwa, hukimbiza mpira haraka na mwepesi kutafuta mpira.”

Baada ya kufanya biashara hiyo kwa sasa Genk, haiwezi kukubali kupoteza mchezaji mwingine zaidi, mwenye uwezo kutokana na kukabiliwa na michuano mingi ikiwa katika mipango kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hivyo kwa vyovyote vile Samatta atalazimika kusubiri, hadi dirisha la usajili la mwakani ndipo afikirie kuondoka katika timu hiyo.

Zaidi ni kwamba biashara ya Samatta kwenda kucheza timu za  England, itanoga baada ya nyota huyo kuonesha cheche zake msimu huu.

Kwani hilo ni miongoni mwa lengo la Genk, kutokana na klabu hiyo kuwa ya kibiashara kwa klabu kubwa Barani  Ulaya na Asia.

Hivyo haitashangaza kumuona Smatta akitua katika moja ya klabu kubwa England msimu ujao, baada ya kushindikana msimu huu.

Miezi miwili iliyopita msaka vipaji Mkuu wa klabu ya Genk,  Roland Janssen  alilamba dili katika klabu ya Manchester United.

Janssen kwa sasa ni muajiriwa katika klabu ya Manchester United na huenda huo ukawa mwanzo wa Samatta, kupiga hatua moja mbele.

Kazi kubwa ambayo skauti huyo amepewa na Manchester United ni kutafuta wachezaji, wanaocheza ligi ya Ubelgiji wenye uwezo mkubwa na kuwaunganisha na mashetani hao wekundu.

Kupata dili kwa skauti, huyo kunaashiria kuwa njia sasa ni nyeupe kwa Samatta kupata nafasi ya kwenda kucheza soka nchini England, kama ataongeza bidii katika kikosi chake cha Genk.

Skauti huyo alikuwa chanzo cha Samatta, kutoka TP Mazembe na kujiunga na Genk na sasa anaweza pia kuwa daraja la kumtoa Genk na kujiunga na Man United ya Jose Mourinho.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe ya Congo, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiibuka kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani, huku kikosi chake hicho kikitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles