23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Salah afikia rekodi ya Ronaldo

MERSEYSIDE, England

KWA kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AC Milan jana, staa wa Liverpool, Mohamed Salah, ameifikia rekodi ya Cristiano Ronaldo ya kupasia nyavu katika mechi saba mfululizo za ugenini kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ronaldo, staa wa Manchester United kwa sasa, aliiweka rekodi hiyo kuanzia mwaka 2013 hadi 2014, wakati huo akiwa mchezaji wa vigogo wa La Liga, Real Madrid.

Mara ya mwisho kwa Salah kutofunga bao katika mechi ya ugenini ilikuwa dhidi ya Ajax mwaka jana, mchezo ambao hata hivyo Liver walishinda bao 1-0.

Aidha, bao la jana lilikuwa la 20, ikiwa ni kwa msimu wa tano mfululizo kumuona mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akifikisha idadi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles