26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Liverpool yaweka rekodi ‘ikiiua’ Milan

MERSEYSIDE, England

KWA kuifunga AC Milan mabao 2-1 jana, Liverpool imekuwa timu ya kwanza ya England kushinda mechi zote sita za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Liver waliandika historia hiyo katika mchezo wa 50 kwa Jurgen Klopp tangu aanze kuiongoza timu hiyo kwenye michuano hii ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).

Katika mechi hiyo iliyochezwa jijini Milan, Italia, Liver ilitanguliwa kwa bao la Fikayo Tomori, kabla ya Mohamed Salah na Divock Origi kujibu majipo kwa kuingia kambani.

Baada ya dakika 90 za mtanange huo wa Kundi B, Mjerumani huyo aliwamwagia sifa wachezaji wake wawili, Alex Oxlade-Chamberlain na Takumi Minamino.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles