27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

SAJNA AKANUSHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

NA SWAGGAZ RIPOTA

BAADA ya kuenea kwa tetesi za staa wa singo ya Iveta, Faraji Twaha ’Sajna’ kutoka jijini Mwanza, kutumia dawa za kulevya kuenea kwenye mitandao ya kijamii, msanii huyo ameibuka na kukanusha vikali taarifa hizo huko akidai yeye ni mtu maarufu hivyo kuchafuliwa ni jambo la kawaida.

Akizungumza na Juma3tata, Sajna alisema ukimya wake wa muda mrefu ulitokana na mabadiliko ya muziki yaliyomfanya ajipange upya na siyo kweli ameingia kwenye janga la kutumia dawa za kulevya kama inavyosemekana kwenye mitandao ya kijamii.

“Hapana sijawahi kutumia na sijui yana asili gani, ninachoweza kusema mimi ni staa kwa hiyo kuzungumziwa vibaya ni moja ya changamoto. Kukaa kimya siyo kutumia dawa za kulevya ila watu wanapaswa kujua kuna maisha tofauti na muziki, yaani nilivyosikia hizo taarifa mpaka  nimekosa nguvu,” alisema Sajna ambaye amewataka mashabiki wake wakae tayari kwa ujio wake mpya baada ya nyimbo zake zilizobamba kama Iveta na Sitaki Kuumizwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles