31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

BARAKA ZAWASHUKIA MASTAA, WAPATA WATOTO MFULULIZO

NA SWAGGAZ RIPOTA

TUMEZOEA kushuhudia rekodi mbalimbali zikiwekwa kwenye tasnia ya burudani, ambapo wasanii na watu maarufu kwenye sekta hiyo wanafanya kazi, matukio na mambo mengine mengi yanayoacha kumbukumbu za kudumu.

Rekodi mpya kwa sasa ni ile iliyowekwa na mastaa wa kike ya kupata watoto mfululizo ndani ya mwezi mmoja huku kila mmoja akiwa na hadithi ya kipekee nyuma baraka hiyo wanayoitamani watu wengi.

Juma3tata tunakusogezea watu hao maarufu walioshiriki kuweka rekodi ya kupata watoto ndani ya mwezi mmoja yaani kutoka Julai 13 mwaka huu mpaka hivi leo Agosti 14.

Millen Magese

Hakuna aliyetegemea kama siku moja Millen Magese anaweza kuitwa mama Kairo, hiyo ilitokana na mrembo huyo kupitia changamoto ya ugonjwa wa ‘Endometriosis’ uliomuweka kwenye hatari ya kutopata mtoto.

Mwanamitindo huyo wa kimataifa na Miss Tanzania mwaka 2001 tayari ameshafanyiwa upasuaji wa kuzibua mirija ya uzazi zaidi ya mara 13 kwenye nchi za Afrika Kusini na Marekani, Julai 21 wengi wakashangaa baada ya kutangaza kuwa Julai 13 mwaka huu alifanikiwa kupata mtoto wa kiume, tukio lililorudisha matumaini kwa wanawake wengine wanaopitia changamoto kama yake.

Linah

Wiki moja baada ya Millen Magese kujifungua, Julai 25 mwaka huu msanii wa Bongo Fleva,  Esterina Sanga ‘Linah’ naye alipata mtoto wa kike ambaye mpaka sasa ameificha sura ya mwanawe huyo.

Kabla hajajifungua Linah aliitikisa mitandao ya kijamii kwa picha zilizopigwa na mpiga picha wa Ben Pol anayeitwa Clemence, zikionyesha amepakwa mafuta mwili mzima na kuonyesha hali yake ya ujauzito.

Faiza Ally

Baada ya siku 8 za kujifungua kwa Linah, Faiza ambaye ni mzazi mweza na mwana Hip hop mkongwe na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjinu, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, mtoto wao wa kike anaitwa Sasha naye alipata mtoto wa kiume.

Agosti 3 mwaka huu alijifungua mtoto anayeitwa Li, ambaye anadai amezaa na mpenzi wake mpya anayeishi Marekani. Kabla ya kujifungua Faiza aliisumbua mitandao ya kijamii kwa picha zake zilizoacha sehemu kubwa ya mwili wazi hasa tumbo lililobeba ujauzito, mtindo unaofanywa na mastaa wengi wanapokuwa kwenye hali hiyo.

Hamisa Mobetto

Siku tano mbele baada ya Faiza Ally kujifungua, mwanamitindo Hamisa Mobetto naye akabahitika kupata mtoto wa kiume na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na usiri alioamua kuuweka mrembo huyo kuhusu baba halisi wa kichanga hicho.

Mobetto ambaye hizi sasa ni mama wa watoto wawili alijifungua Agosti 8 mwaka huu na kuendelea kukabiliana na kiu ya mashabiki wake wanaotaka kumfahamu baba wa mtoto kwani baba wa mtoto wake wa kwanza, Fantansy anafahamika kuwa ni Rdj Majey.

Esha Buheti

 

Rekodi hii ya kipekee inafungwa na staa wa filamu za kibongo, Esha Buheti,  msanii huyu alipishana na siku moja na Hamisa Mobetto kwani naye Agosti 9 alifanikiwa kupata mtoto wa kike katika hospitali ya Sali International iliyopo Msasani, Dar es salaam hivyo kuwa na watoto wawili wakike.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles