29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Sababu ya maumivu wakati, badaa ya ngono kwa wanawake

pix-ii-juu

Na Mwandishi Wetu,

KUNA baadhi ya wanawake huwa na tabia ya kupata maumivu wakati wa kushiriki ngono.

Wataalamu wanasema kuwa hii ni hali inayojitokeza mara nyingi ambapo kitaalamu huitwa dyspareunia.

Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa kushiriki ngono au baada ya kumaliza tendo hilo. Sababu kuu za maumivu haya mara nyingi huwa ni magonjwa ya zinaa na kupungua kwa majimaji ukeni wakati wa ngono.
Mara nyingi maumivu haya huwa kwenye kuta za uke, shingo ya uzazi au chini ya kitovu. Sababu za maumivu haya ni pamoja na kuchubuka ukeni kutokana na maji ya uke kupungua. Inawezekana kutokana na kutoandaliwa vizuri au uke kutotoa majimaji ya kutosha.

Sababu nyingine ni magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia na ‘vaginitis.’ Maambukizi ya shingo ya uzazi (cervicitis)

Nyingine ni maambukizi katika mirija ya uzazi. Mara nyingi maumivu hutokea chini ya kitovu au kiuononi.

Maumivu baada ya tendo

Baada ya kukutana na mwenzi wako kingono, unaweza kuanza kupata maumivu dakika chache mpaka siku kadhaa toka mlipokutana. Maumivu ya kawaida huwa ni kwenye uke kutokana na kuchubuka wakati wa tendo. Unaweza kuyahisi vizuri hasa pale unapojisafisha kwa maji au wakati wa kujisaidia haja ndogo ikiwa njia ya mkojo imechubuliwa.
Maumivu ndani ya uke, kiunoni au chini ya kitovu baada ya kufanya ngono mara nyingi huonesha dalili za maambukizi ya shingo ya uzazi, maambukizi ya mirija ya uzazi na saratani ya shingo ya kizazi.

Dalili hii inaweza kuambatana na hali ya homa, kutokwa damu ukeni baada ya ngono, kutoa uchafu ukeni, kutapika na kichefuchefu.

Matibabu

Wataalamu wanasema kuwa unapopata hali hii mhusika anapaswa kujichunguza vizuri. Kama maumivu hayajatokana na michubuko wakati wa mapenzi, basi ni vema kuonana na daktari haraka iwezekanavyo. Maambukizi ya shingo ya uzazi na mirija ya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease – PID) huchangia kwa kiasi kikubwa hali hii. Matibabu ya haraka ni muhimu ili kupunguza madhara ya magonjwa haya.
Michubuko kutokana na kufanya ngono hupona yenyewe polepole hivyo inashauriwa kutopaka dawa zozote mpaka kupata ushauri kutoka kwa daktari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles