22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Vyakula hatari kwa watoto

soya_beans

Na Mwandishi Wetu,

MTOTO aliye chini ya mwaka mmoja huwa na masharti mno katika masuala ya lishe.

Leo ni vizuri ukajua ni vyakula gani ambavyo mtoto hastahili kulishwa.

Asali – Kwa kawaida inatabia ya kubeba bakteria ambao baadae humwathiri mtoto aliyechini ya miezi 12. Kwa mtoto mwenye umri wa kuanzia mwaka mmoja na kuendelea hawawezi kumwathiri kwa kuwa mwili wake unakinga ya kupigana nao.

Mafuta ya kupikia – Mtoto hahitaji mafuta kwenye chakula chake kwa kuwa vyakula anavyopikiwa vinamafuta ya asilia kama nyama, kuku, samaki iwapo utatumia mafuta, basi ni vema ukatumia ‘butter’ isiyo na chumvi  au olive oil. Haya ni mazuri hayana madhara kama mafuta mengine na yatamsaidia kwenye ukuaji wa ubongo wake.

Soya – Inatengeneza mzio, inapoteza vitamini kwenye mwili wa mtoto hivyo ni vizuri wapewe wakiwa na umri zaidi ya mwaka.

Chumvi – Wazazi wengi wanadhani chakula kisipokuwa na chumvi mtoto hawezi kula, hapana! Yeye ndio anaanza kujifunza kula hivyo hajui ladha yoyote kuwe na chumvi au la! Chumvi ina madini ya sodium ambayo yanaweza kwenda kuathiri figo au kuathiri moyo na kupata matatizo ya shinikizo la damu. Hivyo, haihitajiki chakula kiwe na chumvi hata kama ukitumia basi iwe kiwango kidogo mno.

Sukari – Kiwango kikubwa cha sukari si kizuri kwa watoto kwani inamwaribu meno, fidhi za mtoto huwa katika hatua za kuotesha meno hivyo iwapo atapewa sukari anaweza kuharibu ukuaji wake au mtoto kupata matatizo ya kisukari baadae.

Kwenye uji unaweza kutumia ndizi mbivu ambayo ina sukari ya kutosha kwa kutumia kwa chakula cha mtoto, saga ndizi mbivu halafu changanya kwenye uji  ulioiva ili kupata sukari asilia.

Maziwa ya ngo’mbe – Haya yana madhara zaidi japo jamii imeshazoea kuwapatia watoto. Maziwa yana protini nyingi mno ambayo mtoto hawezi kumudu kuisaga hivyo baadaye husababisha madhara kwenye ini. Pili yana sababisa mzio (allergy) kwa watoto, ukiona kila unapompa anatapika au kuharisha ni heri ukamwachisha kwani ukiendelea itatengeneza mzio na baadae atashindwa kutumia.

Vyakula vibichi – Vinaweza kumpatia bakteria, usipende kumpa mayai mabichi, nyama au samaki (sushi).

Vyakula vyenye mafuta kwa wingi – Hivi ni kama chips, crips, burger, keki, chocolate, mabisi au ice cream, si vizuri kwa watoto.

Samaki wenye madini ya zebaki (mercury) nyingi –Mfano wa samaki hawa ni papa, chuchunge, dagaa wakubwa na wengineo. Wana tabia ya kuathiri mfumo wa neva. Badala yake mpe sangara, sato au salmon, hawa wana mafuta ya kutosha na omega 3 zitakazo msaidia kukuza ubongo na kumfanya kuwa na akili.

Njugu – vitu kama karanga au korosho mtoto asipewe kutafuna vinaweza kumkwama kooni. Kama ni karanga basi iwe ni ya kusagwa na wapewe watoto kuanzia miezi sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles