Odegaard asifia muziki wa Rashford

0
1660
Marcus Rashford
Marcus Rashford
Marcus Rashford

LONDON, ENGLAND

KINDA wa Real Madrid, Marin Odegaard, juzi alikiri kufunikwa na kiwango cha kinda wa Manchester United, Marcus Rashford.

Kauli ya Odegaard ilitokana na kiwango cha Rashford ambaye anacheza katika timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 nchini England, kufunga ‘hat  trick’ katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi  ya Norway mchezo uliochezwa juzi  uwanja wa Community England.

Odegaard hakuwa katika kiwango kizuri kwenye mchezo huo ambao alishuhudia timu yake ikishindwa kuzuia kasi ya Rashford ambaye alionekana kuwa katika kiwango bora zaidi.

Kiwango hicho kilifanya Odegaard ambaye alikuwa mara yake ya kwanza kucheza katika ardhi ya England amsifu   Rashford kutokana na uwezo wake uwanjani.

“Ni miongoni mwa wachezaji wa kiwango bora  niliowahi kuwaona katika soka pia Rashford aliwahi kuonesha  kiwango hicho akiwa Ligi Kuu England,” alisema Odegaard.

Odegaard alisema angependa siku moja acheze pamoja na  nyota huyo kati ya Manchester United au Real Madrid.

“Ni vizuri kucheza na mchezaji anaye kuvutia uwanjani,” alisema Odegaard.

Akizungumzia kiwango chake Madrid alisema anajitahidi kuhakikisha anacheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

“Natarajia nitapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza hivyo najituma kuhakikisha lengo langu linatimia,” alisema Odegaard.

Nyota huyo aliongeza kwamba, bado umri wake wa miaka 17 unaruhusu kujifunza zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here