Arsene Wenger akoleza bifu na Mourinho

0
914

1412518674652_wps_19_arsene_wenger_manager_hea

ENGLAND, LONDON

UPINZANI wa muda mrefu kati ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na wa Manchester United, Jose Mourinho,  unatarajia kuongezeka msimu huu baada  juzi Wenger kukataa kukaa karibu na  mpinzani wake huyo katika mkutano wa makocha ulioandaliwa na Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (UEFA) jijini London, England.

Makocha hao walijikuta wakiendeleza mgongano hata nje ya uwanja, huku kocha wa United, Mourinho, akijikuta katika wakati mgumu zaidi kwa uamuzi wa Wenger kugoma kukaa siti ya karibu naye.

Ilidaiwa kwamba tangu Mourinho  ajiunge kuwa kocha mpya wa  Manchester United, amekuwa katika hali  ya utulivu jambo ambalo limesaidia kupunguza mvutano dhidi ya Wenger. Hata hivyo, kocha huyo ambaye hivi karibuni alishinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Agosti mwaka huu ya Ligi Kuu England, alionekana akitabasamu muda wote huku akikumbatiana na wafanyakazi wa UEFA pamoja na makocha wenzake.

Katika mkutano huo, Mourinho alikuwa wa mwisho kuingia katika chuma cha mkutano huo kabla ya kukutana na  kocha wa zamani wa timu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson.

Kwa mujibu wa mtandao wa Marca,  wakati kocha huyo akiingia ukumbini humo kulikuwa na siti chache tupu  ambapo mbele ya siti hizo walikuwa  wamekaa kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane na wa PSG, Unai Emery, hivyo Mourinho aliomba kukaa  siti mojawapo ambayo haikuwa na mtu.

“Hapana haiwezekani,” alisikika Wenger, bila kusita wakati alipogundua Mourinho alikaa karibu yake.

Ilifahamika kwamba, kitendo hicho kilionekana na makocha wengine katika ukumbi huo ambao hawakutaka   kujionesha walikuwa wakifuatilia mzozo huo.

Msuguano wa makocha hao inasemekana  ulianza tangu mwaka 2004 wakati Mourinho akijiunga kuwa kocha wa  timu ya Chelsea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here