23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ruangwa yapongezwa kuanzisha Tehama kwa bodaboda

NA HADIJA OMARY, LINDI

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021, Luteni Josephine Mwambashi,  ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kwa kuendelea kuwalinda vijana wanaotumia vyombo vya moto kwa kuwaanzishia mfumo wa TEHAMA (Tracking system) utakaoweza kuratibu matumizi pamoja na usalama wa waendesha bodaboda.

Luteni Mwambashi ameyasema hayo leo baada ya mwenge wa Uhuru kutembelea katika kikundi cha vijana waendesha pikipiki na bajaji wilayani hapo.

Kiongozi huyo alipokea taarifa ya ukopeshwaji wa pikipiki na bajaji pamoja na matumizi ya mfumo wa Tehama uliowekwa katika vyombo hivyo vya usafiri vilivyokopeshwa

Amewapongeza kwa kuitumia Tehama kikamilifu kwa kuwa ndio ujumbe mkuu wa mbio maalum za mwenge wa Uhuru 2021 unahusu matumizi sahihi ya Tehama.

“Niwapongeze kwa kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwenge wa Uhuru uliobeba ujumbe usemao Tehama ni msingi wa Taifa endelevu, tuitumie kwa usahihi  na uwajibikaji.

“Tumeona wana Ruangwa ni kwa namna gani tunaitumia teknologia hii kuhakikisha kwamba tunalinda vijana wetu na vyombo hivi vya moto,” amesema Mwambashi.

Akitoa taarifa ya mfumo huo  kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, msimamizi wa kikundi cha bajaji na pikipiki, Mwinyi Jalala  amesema kuwa lengo la  ufungaji  wa mfumo wa Tehama ni kuratibu matumizi ya vyombo hivyo vya usafiri na usalama wa vijana  wanaoendesha vyombo .

Amesema bajaji na piki piki zilizoingizwa kwenye mfumo wa Tehama ni zile zilizotelewa kwa mkopo kwa vijana wa halmashauri hiyo kutoka katika asilimia 10% ya mapato ya makusanyo yao ya ndani.

Amebainisha kuwa kufungwa kuwa mfumo huo katika vyombo hivyo vya usafirishaji kunaweza kusaidia kugundua piki piki ilipo  mahali gani na wakati gani endapo chombo hilo kitaibiwa

“Kama tunavyojua hivi sasa wizi wa vyombo hivi vya usafiri ni mkubwa sana hivyo kwa kutumia mfumo huu tunaweza kubaini kwa haraka pikipiki ama bajaji ilipo kama ikitokea imeibiwa na tutaweza kuifuatilia na kuipata,” amesema.

Nae Mkuu wa Idara ya Tehama katika halmashauri hiyo, Jitete Mbonde amesema kuwa mfumo huo kwa sasa unatumika kupitia simu ambapo mtaalamu anaweza kuona mienendo yote vya vyombo hivyo vya usafiri kwa kutambua sehemu iliyopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles