23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga ya Manara, Azam FC ya Dk. Tiboroha, kupanga ni kuchagua!

Na Hassan Daudi, Mtanzania Digital

YAPO mengi lakini kwa wiki chache za hivi karibuni, macho yangu yameangukia kwenye mambo mawili makubwa yaliyojitokeza kwenye soka la Tanzania.

Achana na usajili wa klabu mbili kubwa nchini, Simba na Yanga. Hapana. Azam FC wameajiri Mkurugenzi wa Ufundi (Dk. Jonas Tiboroha) huku Yanga wakiajiri Msemaji (Haji Manara)… Si mbaya, maana kila upande umeamua kuboresha pale ulipohisi kuna udhaifu.

Haji Manara baada ya kujiunga na Yanga hivi karibuni.

Lakini sasa, ni ushahuri tu, kwamba Yanga haionekani kuwa na shida sana kwenye ishu ya ‘ushawishi’.

Kwa maneno mengine pasi na kubadili maana, ujio wa Manara haukuwa na tija sana, kama ambavyo wangempata mtu aina ya Dk. Tiboroha.

Kwa kiwango cha ushawishi wa Yanga kwenye soka la Tanzania, hata kama ishu ya ‘branding’ ingehitaji maboresho, basi naamini wangelazimika kupata mtu kutoka Al Ahly, Wydad Casablanca, Zamalek, au Mamelodi Sundowns, na si Manara aliyekuwa Simba.

Ukija kwa Azam FC, hata baada ya kumpata Dk. Tiboroha, bado ilimuhitaji mtu aina ya Manara kwa kuwa ushawishi wa klabu hiyo mbele ya mashabiki wa soka nchini ni mdogo licha ya uwekezaji mkubwa wa mzee Bakhresa.

Hata hivyo, huenda Azam FC wameamua kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Kwamba matokeo ya uwanjani yatakayotokana na kazi ya Dk. Tiboroha yatawavusha kwenye kizingiti cha ushawishi kwenye soka la Tanzania.

Mwisho, kupanga ni kuchagua. Kila upande umefanya kile ulichoona kina tija kwake. Hongera kwa Yanga ya Manara, pia pongezi kwa Azam FC ya Dk. Tiboroha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles