ROONEY MAANA HALISI YA UAMINIFU SI TAMAA YA FEDHA

0
707

 

ADAM MKWEPU NA MITANDAO


MCHEZAJI wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, amekuwa kielelezo tosha cha kutofautisha kati ya mchezaji  mwenye tamaa ya fedha na yule mwaminifu  wa mapenzi yake kwa klabu iliyomlea.

Wiki iliyopita Rooney alikuwa gumzo Ukanda wa Afrika Mashariki na kati baada ya kutua nchini Tanzania na kuiongoza vema klabu yake ya Everton kupata ushindi wa mabao 2-1, katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Rooney, alifunga bao lake la kwanza baada ya miaka 13 tangu ahame klabu hiyo akitokea Manchester United.

“Nimetunza siri hii kwa miaka zaidi ya 13,” anasema Rooney baada ya kujiunga na Everton na kuongeza: “Lakini miaka yote hiyo nimekuwa nikivaa nguo za Everton na watoto wangu.”

Ujumbe huu uliwastaajabisha mashabiki wa Everton kwani nyota huyo aliondoka katika klabu hiyo mwaka 2004 na kubaki kuwa shabiki kama ambavyo mwenyewe anakiri: “Nimekuwa shabiki wa klabu hii tangu nikiwa mdogo.”

 

Rooney amerejea akiwa na kumbukumbu inayoendelea kuumiza kichwa chake akiwa na majina ya wale wote waliohusika katika anguko lake.

Maadui zake walimshuhudia Uwanja wa Old Trafford akiwa nahodha ambaye hakutakiwa kucheza mchezo mkubwa wakati timu yake inapokuwa kwenye mapambano.

Wasiompenda waliimba na kucheka kwa furaha wakitamka kwa kulikebehi jina la Rooney kwa kumwona mchezaji asiyefanana na yule wa awali amepotea, uwezo wake umeshuka anachosubiri ni kutundika daruga.

Dharau na kebehi hizo zinaweza kuwa sababu kwa wengine kutaka kujikumbusha zamani wakati nyota huyo ambaye amerejea Everton kama mchezaji huru, akiwa kijana kabla ya kusajiliwa kwa pauni milioni 27 mwaka 2004.

Acha tuwe na matumaini kwamba stori ya Rooney kuvaa nguo za Everton wakati akiwa mchezaji wa Manchester United, kulionesha mapenzi ya kweli kwa klabu yake ya zamani.

Unaweza kumweleza Rooney au mchezaji yeyote kwamba kuigiza kama  shabaki wa muda mrefu wa klabu flani ni ujinga.

Lakini jambo hilo halitakiwi kuonekana moja kwa moja kwa kuwa linasukumwa na tamaa ya mashabiki ambao wanaumia zaidi wanapogundua kuwa nyota aliyehamia katika timu yao ana mapenzi na klabu nyingine.

Kwa kawaida mchezaji anapokuwa wa kulipwa, anaacha kabisa kufikiria suala la kuwa shabiki wa klabu Fulani, hivyo katika viatu vyake kunakuwa na dhamira nyingi.

Rooney alizaliwa katika familia yenye mapenzi na Everton na alitakiwa  kupewa  jina la Adrian mwaka 1980 kwa kuwa huyo alikuwa shujaa wa kipindi hicho.

Ameanza kwenda kutazama mechi za Everton Uwanja wa Goodison akiwa na miezi sita yaani wazazi wake walimfanya kuwa shabiki wa timu hiyo tangu akiwa mtoto.

Rooney akiwa na miaka tisa aliwahi kumwandikia barua mshambuliaji wa kati wa timu hiyo wakati huo akiwa Duncan Ferguson, akimweleza hakutakiwa kuwa mfungwa.

Kuna wakati Rooney akiwa na miaka tisa, aliwahi kufanya majaribio Liverpool huku akiwa amevaa nguo za Everton, hakuona jambo la ajabu kwa kuwa aliamini Everton ni familia yake.

Liverpool walimpenda na walimhitaji kufika hapo baada ya wiki, lakini kabla kutimia Everton walimpa ofa ya kusoma katika shule yao na tangu hapo alikuwa mchezaji wa klabu anayoipenda katika maisha yake.

“Liverpool kusikia hivyo walinitaka nisaini hata kabla ya kumaliza majaribio yangu, jambo ambalo kama ningesaini ningekuwa miongoni mwao hadi sasa,” anasema Rooney.

Wachezaji wengine wa zamani ambao ni mashabiki wa kutupwa wa Everton, kama Robbie Fowler, Steve McManaman na Jamie Carragher wamepitia katika hatua hizo.

Zaidi ni kwamba hata wachezaji wadogo hawafikirii kuhusu kuwa shabiki, badala yake hujiona ni wachezaji na wanapambana ili kuwa wachezaji wa kulipwa; hilo ndio lengo lao kubwa.

Lakini kwa Rooney bado alikuwa na tabia za kishabiki hata alipokuwa mchezaji wa kulipwa. Baada ya kufunga na kuiongoza Everton katika fainali ya Kombe la FA la vijana mwaka 2002, alishangilia kwa kuvaa fulana iliyoandikwa ‘Atabakia kuwa Blue kila siku.’

Lakini hata mchezaji ambaye alianza kuwa kama shabiki, taratibu anaweza kuwa mwajiriwa wa klabu husika.

Tukimnukuu Ashley Cole ambaye ni kipenzi cha Arsenal ansema: “Uamuzi wa kuwa karibu na klabu unayoipenda unapata ya kujifunza na kuwajua mashujaa waliopita.”

Soka la kulipwa limekuwa na roho mbaya sana kwa kuwa linajali ulinzi na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na klabu itawatunza wachezaji wake kama bidhaa ya kuuza na kununua.

Kwa mara ya kwanza Rooney anasaini mkataba wa mchezaji wa kulipwa Everton, aliyaona hayo akiwa mbele ya watu 100,000 na zaidi ya camera 12 ambazo zilishuhudia kinachoendelea uwanjani.

Kuna wakati alijiona bado mchezaji wa kawaida kwa kuhitaji kuendelea kunywa maji bila glasi, jambo ambalo lilimkera sana David Moyes ambaye wakati huo alikuwa kocha wake.

Mchezaji kama Frank Lampard, alipata shida sana alipokuwa West Ham baada ya mashabiki kusema kuwa hana mapenzi na klabu hiyo.

Ndio, kuna wachezaji ambao hawana mchezo na klabu zao na hawapendi kuziacha, kwa mfano  Paolo Maldini, Philipp Lahm, Xavi, Paul Scholes au Ryan Giggs.

Wachezaji hawa ni waaminifu kwa klabu zao.

Lakini ni vema kusema walikuwa waajiriwa wazuri kwa waajiri wao, walicheza na kulipwa fedha nyingi katika klabu zao lakini kwanini waliamua kuachana nazo na kuondoka?

Ukiwauliza watakwambia kuwa walikuwa wachezaji wa kulipwa ambao walikuwa na kazi, kama ambavyo wajuzi katika shughuli nyingine ambao wanatamani mafanikio.Wachezaji wa aina hiyo wanaamini kama watapata mafanikio, fedha zitawafuata.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here