WABUNGE WADAI NASA IKISHINDA MIRADI ITAKUFA

0
578

NAIVASHA, KENYA


WABUNGE 12 wa Chama cha Jubilee wameeleza hofu yao kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ya Jubilee huenda ikasitishwa iwapo muungano wa NASA utashinda Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8.

Chini ya vugu vugu la Uhuruto Express,wabunge hao walitaja miradi, ambayo huenda ikaathirika kuwa pamoja na ijenzi wa reli ya kisasa ya SGR hadi Naivasha.

Wabunge hao kutoka sehemu mbali mbali nchini walitoa wito kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi kuipigia kura serikali ya Jubilee.

Hayo yaliibuka baada ya wabunge hao kuzuru vituo kadhaa vya kibiashara  huko Naivasha  na Gilgil kumpigia debe Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Wakati wa ziara hiyo, wabunge hao walishutumu ghasia zinazoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo nchini wakiongeza kuwa kila mwanasiasa ana haki ya kufanya kampeni zake kokote nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here