27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

RIDHIWANI ALILIA UMEME CHALINZE

NA GUSTAPHU HAULE – PWANI


MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM), amemwomba Waziri wa Nishati na Madini, Professa Sospeter Muhongo, kutoa kipaumbele kwa kufikisha umeme katika vijiji vilivyopo kwenye jimbo lake ili kuwasaidia wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Ridhiwani alitoa ombi hilo juzi wakati akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu uliofanyika katika Mtaa wa Misufini katika Halmashauri ya KibahaVijijini.

Alisema jimbo lake lina vijiji 63 na vitongoji 19, lakini mpaka sasa vilivyopata umeme ni  42 lakini katika mradi huo wa awamu ya tatu, ameahidiwa vijiji vingine 14 kufikiwa, huku akiomba suala hilo lifanyike haraka ili mwaka 2020 iwe rahisi kwake kushinda ubunge.
 

“Mheshimiwa waziri nashukuru katika mradi huu wa REA awamu ya tatu nimeambiwa vijiji vyangu 14 vitanufaika, lakini mimi naomba mchakato huo ufanyike mapema ili mwaka 2020 ninaporudi kwa wananchi nipate la kusema,” alisema.

Aidha, mbunghe huyo alisema mahitaji ya umeme bado ni makubwa katika jimbo lake kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka, huku akitolea mfano Kata ya Kiwangwa ambayo awali ilikuwa na kaya 81 zilizokuwa zikihitaji nishati ya umeme, lakini kwa sasa imefikia 280 jambo ambalo linapaswa kuangaliwa upya.
 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, alisema mahitaji ya umeme yanazidi kuongezeka kutokana na kasi ya ukuaji wa viwanda na kwamba kwa sasa mkoa unapata megawat za umeme 38 mpaka 40 ambazo hazitoshelezi.
Kwa upande wake, Profesa Muhongo alisema katika mradi huo wa REA awamu ya tatu, wanufaika wakubwa ni wananchi wa Mkoa wa Pwani na kwamba utekelezaji wa awali utapitia vijiji 55 vikiwemo 14 vya Chalinze.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles