29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

RICO SINGLE, BABY J WAUNGANA

BAADA ya kufanya shoo nzuri kwenye tamasha la Zanzibar Swahili Ukumbi wa Ngome Kongwe visiwani hapa, wasanii wawili wa Bongo Fleva, Jamilah Abdulah (Baby J) na Rico Single, wameamua kuungana na kufanya kolabo ya wimbo wao mpya utakaotoka ndani ya mwaka huu.

Wasanii hao maarufu Zanzibar, walisema licha ya kuwahi kuimba wimbo wa pamoja miaka ya nyuma mwaka huu wameamua kukaa pamoja kutengeneza wimbo utakaofungua milango ya muziki wa Zanzibar kwenye soko la kimataifa.

“Unajua sisi tuna mashabiki wengi hapa Zanzibar hata na bara sasa tumeona tuandae wimbo wa pamoja kwa ajili ya kukuza muziki wetu wa Zanzibar kimataifa na pia tutengeneze njia nzuri ya ushirikiano kwa wasanii wengine hapa Zanzibar,” alisema Baby J maarufu mrithi wa Bi Kidude.

Naye Rico Single, alisema muziki wa Bongo Fleva kwa sasa umekuwa mno tofauti na zamani ulivyokuwa ukichukiwa na wazee.

“Zamani wazee hawakuutaka kabisa muziki wa Bongo Fleva, lakini sasa wanauimba hivyo tukifanya kolabo na Baby J itaongeza hamasa kwa watu wa rika zote na pia tutawaleta mashabiki wetu pamoja na tutakuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wasioelewana wao kwa wao,” alisema Rico Single. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles