23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

WAFUNGWA WAPALESTINA WAANZA MGOMO WA KULA ISRAEL

YERUSALEM, ISRAEL


MAMIA ya Wapalestina walio katika jela za hapa wameanza kususia chakula wakilalamikia mazingira duni magerezani.

Hatua hiyo inaongozwa na Marwan Barghouti, Kiongozi wa Palestina aliyehukumiwa maisha kwa makosa matano ya mauaji.

Barghouti, ambaye ana ushawishi mkubwa ndani ya Chama cha Fatah kinachoongozwa na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, anasemekana kuwa na nafasi kubwa ya kumrithi Abbas.

Inahofiwa kuwa mgomo huo unaweza kuchochea ghasia katika eneo linalokaliwa na Israel katika Ukingo wa Magharibi

Kwa mujibu wa Idara ya Huduma za Magereza Israel, Wapalestina 1,187 walio kizuizini wanaunga mgomo huo, ambao umeenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wafungwa wa Palestina.

Suala la Wapalestina kufungwa katika jela za Israel limekuwa la mvutano kati ya pande hizi mbili.

Wapalestina walio kizuizini kama wafungwa wa kisiasa, wengi wao ni wale waliohukumiwa kwa mashambulizi dhidi ya Israel.

Wengine wanashikiliwa kwa kile kilichotajwa kama kuzuiliwa kiutawala, sharia, ambayo inakubali washukiwa kuzuiwa bila kusomewa mashtaka kwa muda wa miezi sita.

Kuna Wapalestina 7,000 walio vizuizini katika jela za Israel kufikia mwisho wa mwaka jana, kwa mujibu ya makundi ya wafungwa wa Palestina.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles