23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Remtullah:Naomba Serikali ipunguze bei za malighafi

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

MBUNIFU wa mavazi  nchini, Ally Remtullah, ameiomba Serikali kupunguza bei za malighafi  za  kutengenezea nguo ili watu waendelee  kupenda vya nyumbani zaidi.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Remtullah amesema anawapongeza  wadau mbalimbali wanaoendelea kutoa ushirikiano na kununua kazi za wabunifu hao hususani viongozi,wasanii pamoja na wanamichezo.

 “Sheria ngowi amebuni jezi ya timu ya Yanga ni kitu kizuri kwa namna moja au nyingine inaonyesha wazi kuwa wabunifu tunaendelea kupewa nafasi katika jamii lakini ingependeza zaidi jezi hiyo ingetengenezwa hapa hapa nchini ila kutokana na kuwepo kwa shida ya baadhi ya malighafi imelazimika jezi hiyo kutengenezwa nje ya nchi,” amesema.

Amesema kwa sasa amejikita zaidi kusaidia wabunifu chipukizi  kupitia darasa lake alilolipa jina la “Remtulah 010 ” ikijumuisha wabunifu wakubwa pamoja na watoto.

“Ni darasa ambalo linafanyika kwa miezi mitatu yenye vitendo na ninawapa nafasi kuwaandalia jukwaa la kuonyesha kazi ama vitu ambavyo wamebunia kuanzia watoto pamoja na wakubwa na katika darasa hilo watoto ni bure kabisa hakuna malipo,” amesema

Amesema kupitia darasa hilo linampa nafasi mkufunzi kujitangaza kibiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles