31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Son aibua presha Tottenham

TOTTENHAM wamepata pigo baada ya mshambuliaji wake raia wa Korea Kusini, Son Heung-Min, kupata majeraha ya kigimbi cha mguu akiwa na timu yake ya taifa.

Nyota huyo ameumia akiwa mazoezini na itakumbukwa alicheza kwa dakika zote 90 za mchezo wa suluhu dhidi ya Iraq.

Ni kwa majeraha hayo, Son mwenye umri wa miaka 29 ameachwa kwenye kikosi kitakachoivaa Lebanon usiku wa leo.

Tangu msimu huu wa Ligi Kuu England uanze, Son amekuwa kwenye kiwango cha juu ambapo alifunga mabao ya ushindi katika mechi dhidi ya Man City na Watford.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles