24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ramadhan Brothers wapokewa kwa kishindo Dar

Na Christopher Msekena, Mtanzania Digital

Wasanii wa sarakasi kutoka Tanzania, Ibrahim na Fadhili Ramadhan wanaounda kundi la The Ramadhan Brothers wamereja Tanzania leo Machi 08,2024 wakitokea Marekani ambako hivi karibuni walishinda katika mashindano ya kusaka vipaji ya ‘America’s Got Talent Fantasy League’ na kujinyakulia Dola 250,000 (Sh milioni 637.5) pamoja na tuzo.

Wasanii hao ambao wamepokelewa na Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na BASATA, wametua Uwanja wa Ndege wa Mwl. JK Nyerere Dar es Salaam ambapo ndege waliyosafiri nao imemwagiwa maji (water salute) ikiwa ni ishara ya heshima kwa Wasanii hao kwa kuiheshimisha na kuitangaza Tanzania.

Mashindano ya ‘America’s Got Talent’ yalianza rasmi mwaka 2006 ambapo dhamira yao kubwa ilikuwa ni kusaka vipaji kwenye nyanja mbalimbali Marekani kabla ya baadaye kupanua wigo na kuvisaka vipaji vya maeneo mbalimbali Duniani ambapo kwa mwaka huu 2024 mashindano hayo yamefanyika kwa utofauti kidogo kutokana na Majaji kupewa nafasi ya kuwarudisha Washiriki waliopita katika misimu iliyopita kisha kuwapatia nafasi ya kushindanishwa upya ili kuwania kitita cha $250,000 pamoja na tuzo.

Ramadhani Brothers ambao walishiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza mwaka 2023 kwenye msimu wa 18 wa America’s Got Talent na kushika nafasi ya 5, wamewahi pia kushiriki mashindano mengine ya kimataifa katika Nchi za Ujerumani, Slovakia, Ufaransa , Australia pamoja na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles