23.1 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Aja T Limited awataka wanawake kuchangamikia fursa ya biashara Afrika

Na Ester Mnyika, Mtanzania Digital

Mkurungenzi wa Kampuni ya Aja T.Limited , Happiness Nyiti ambaye ni mfanya biashara katika soko la Eneo Huru la Biashara Afrika, ametumia maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani inayofanyika kila mwaka Machi 8, kuhumiza wanawake kufanya biashara katika soko huru.

Hapiness pia ni mmiliki wa kampuni ya Tanzania Sisal Fiber co Limited iliyopo nchini Morocco ambayo inajihusisha na uuzaji wa nyuzi za mkonge.

Amesema wanawake wanapaswa kuwa na uthubutu wa kufanya biashara katika soko la hilo kwa sababu kuna fursa nyingi ambazo zinapatikana.

Amesama kwa sasa wanatafuta wanawake ambao wapo tayari kuingia katika soko hilo ili kutengeza msingi wa pamoja ambao utawawezesha kujua taratibu ya kufanya biashara nje ya nchi ikiwemo sheria mbalimbali na fursa zilizopo.

“Juhudi anazofanya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kufungua fursa katika mataifa mbalimbali ikiwemo Eneo Huru la Biashara Afrika hii ni kwa ajili yetu wanawake ambao tunajishughulisha na biashara, mama amefungua milango ili tuweze kufanya biashara zetu Afrika ,” amesema Happiness.

Anasema kuwa yeye ni mmoja wa watu waliofaidika na biashara katika soko hilo, hivyo kuwataka wanawake kuwa bidhaa zenye ubora na kukidhi vigezo ambavyo vinahitajika kimataifa.

Ameeleza kinachohitajika katika soko ni uhakika wa bidhaa na usambazaaji kwa wakati ili upatikanaji uwe rahisi kwa mteja anapohitaji bidhaa na anapata kwa wakati bila changamoto yoyote.

“Kwa sasa hivi wanawake wa Tanzania kuna fursa kubwa kwa sababu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk.Ashantu Kijaji ni Mwenyekiti wa Mawaziri walio chini ya mkataba wa soko hili ni dhahiri wanawake tunaweza kufanya biashara katika soko hili,”amesema.

Amesama kwa sasa hali ya biashara katika s ni nzuri na milango iko wazi, wanawake wanatakiwa kuamka karne hii ni ya kujishughulisha na biashara, kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na kuchangia pato la Taifa.

Happiness anasema kuna mnyororo wa thamani ambao wanawake wengi wapo humo ndani ambao wanawawezesha wanawake wenzao kufanya biashara kuvuka mipaka katika soko hilo, mfano katika biashara ya mkonge wanawake wanahusika katika kuchambua, kupanga, kuandaa nyuzi za Mkonge ni ongozeko la ajira kwa wanawake.

Amesema Tanzania kuna rasirimali nyingi ambazo nchi nyingine hakuna, kuna fursa mazao ya kilimo,madini, misitu na sanaa na ubunifu,hivyo wanawake wanapswa kutumia fursa hizo kuuza bidhaa hizo.

“Wanawake wakizalisha bidhaa zitokanazo na rasirimali zetu tunaweza kuuza bidhaa zetu kwa wingi, soko hili fursa ni kubwa inapasa kutumia fusra hizi kwa sababu Rais Dk. Samia ametengeneza mazingira rafiki ya ufanyaji biashara nje ya mipaka ya Tanzania,”anasema.

Amesema sio tu kupeleka bidhaa katika nchi zilizopo kwenye Eneo Huru la Biashara Afrika pia wanafursa ya kuingiza bidhaa za nje ya nchi ambazo zipo kwenye makubaliano ya soko hilo, hivyo fursa muhimu kwa wafanyabiashara wanawake nchini.

Amefafanua kuwa wanawake ndio nguzo wakifanya vizuri katika soko hilo kunawawezesha vijana kuingia katika soko hilo kwa urahisi na kuwasaidia kuwapa elimu, ujuzi na kuwashika mkono na itaongeza ajira kwa vijana wanaotoka vyuoni.

Happiness amesema kutokana uhitaji wa soko hilo watawawezesha wajasiriamali kutengeneza bidhaa zinazo kidhi viwango kutengeneza soko ambalo watanufaika nalo.

“Kutokana mitaji yetu kuwa midogo wanawake wanatakiwa kuungana katika vikundi ili iwe rahisi kufanya biashara kwa urahisi na kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa katika soko hilo itakuwa tumesaidia kuinua uchumi wa nchi yetu,”amaesema.

Amesema umoja wa wanawake ndio utakao wapeleka mbele zaidi katika soko hilo wakishirikiana na kusaidiana katika mambo mbalimbali, wakati huu sio wa kujaribu ni kufanya kwa kutenda na wamefikia ngazi ya uongozi na kuna wanawake wafanyabiashara wakubwa.

Aidha amesema wanawake kutumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zao katika soko hilo utumiaji mzuri wa mitandao hiyo huleta fursa katika soko.

Ameongeza kuwa waanawake wanatakiwa kufanya kazi hata kama hakuna mtaji wa biashara lazima washughulike kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao na changamoto wanazokutana nazo ndio fursa wakiangalia kwa jicho chanya wasikate tamaa.

“Wekeza katika kufanya kazi au kutengeneza bidhaa nzuri ambayo itauzika sokoni sio kuangalia pesa kwanza, kabla hujawekeza kwenye bidhaa ambayo itawavutia wateja na kuwajengea imani wateja kwa bidhaa yako ,”amesema.

Amewashauri wanawake kuchangamkia fursa zinapotokea kwa wakati na kutafuta taarifa sahihi katika fursa hiyo na pia wasijiwekee kipimo katika kujifunza mambo mapya maana ni hazina na kutokuchagua aina ya kazi au kuangalia ngazi ya elimu aliyonayao katika kufanya kazi au biashara.

Happiness ameishukuru wizara ya viwanda na biashara kwa ushirikiano na juhudi wanazofanya kunyanyua wanawake na kuwapatia fursa zitakanazo na soko hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles